Kamanda wa kikosi cha amani cha
Umoja wa Afrika katika Jamhuri ya Afrika ya Kati anasema askari wake
wameukomboa mji wa Sibut, baada ya kutekwa na wapiganaji wa zamani wa
Seleka.
Kamanda huyo, Jenerali Tumenta Chomud, alisema
askari kutoka Gabon sasa wako mjini Sibut, na watawanyang'anya silaha
wapiganaji waliouteka mji huo Alkhamisi.Wapiganaji wa zamani wa Seleka - wengi wao Waislamu - wamekuwa wakiondoka mji mkuu, Bangui, ambao uko kama kilomita 200 kusini ya Sibut.
Kuondoka kwa Seleka kumezusha mauaji ya kulipiza kisasi, na watu zaidi ya 40 wameuwawa mjini Bangui katika siku chache zilizopita.
0 comments:
Post a Comment