pagead2.googlesyndication.com pagead2.googlesyndication.com
Showing posts with label TRANSPORT. Show all posts
Showing posts with label TRANSPORT. Show all posts

Ndege ya kwanza ya Magufuli yatua Dar


NDEGE mpya ya kwanza iliyonunuliwa na serikali kwa ajili ya kutumiwa na Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL), imetua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam (JNIA), ikitokea nchini Canada ilikotengenezwa.
Ndege hiyo ilitua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere majira ya saa 6:15 mchana jana. Baada ya kutua ndege hiyo, ilipatiwa heshima maalumu ambayo hutolewa kwa ndege yoyote mpya inayotua katika nchi yake (Water Salute) na kisha kuegeshwa katika eneo la ndege za jeshi (Airwing Ukonga).
Akizungumza baada ya kuwasili kwa ndege hiyo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dk Leonard Chamriho alisema ndege ya pili inatarajiwa kuwasili baada ya wiki moja.
“Baada ya kuwasili ndege ya pili ndipo yatafanyika mapokezi rasmi, yatakayoongozwa na Rais Magufuli kwa tarehe itakayotangazwa baadaye,” alisema Chamriho.
Taarifa ya awali iliyotolewa na ATCL mwishoni mwa wiki, ilieleza kuwa ndege hiyo yenye uwezo wa kubeba abiria 76 ikiwa na marubani wanne kutoka Canada, ilianza safari ya kuja nchini tangu wiki mbili zilizopita ikipitia miji ya Reykjavík, Southampton, Malta, Luxor na Addis Ababa Ethiopia. Ilieleza kuwa ndege hizo, zitaanza kufanya safari zake mara tu baada ya kukamilisha mchakato wa kusajiliwa na Mamlaka ya Usalama wa Anga Tanzania (TCAA).
“Kwa kuwa zitakuja zikiwa na usajili wa nchini Canada, tutalazimika kutumia siku mbili hadi tatu kuziingiza kwenye usajili wa TCAA pamoja na kukamilisha taratibu nyingine za kisheria ili ziweze kupata ruhusa ya kufanya safari za hapa kwetu,” ilieleza.
Iliongeza kuwa safari ya kwanza ya ndege hiyo, inatarajiwa kufanyika Septemba 27, mwaka huu kwenda jijini Mwanza.
“Tutakuwa na madaraja mawili yaani daraja la uchumi (Economy Class) litakalohusisha abiria 70 na daraja la biashara (Business Class) litakalohusisha abiria sita kwa kila ndege,’’ ilibainisha. Ilitaja baadhi ya maeneo ambayo shirika hilo litaboresha zaidi safari zake kuwa ni Dodoma, Mwanza, Arusha, Mbeya, Kigoma, Tabora, Mpanda, Kilimanjaro, Mtwara, Zanzibar, Pemba, Bukoba na Visiwa vya Comoro. Ujio wa ndege hizo unatajwa kuwa utaleta mapinduzi makubwa kihuduma na kiutendaji kwa shirika hilo.
Tayari kampuni hiyo imebainisha kwamba imeunda kikosi kazi, kinachosimamia masuala mbalimbali likiwemo suala la mafunzo ya watendaji wake mbalimbali ili kuendana na matakwa ya biashara hiyo kwa sasa likiwemo suala la kufanya biashara kwa ushindani. Ujio wa ndege hizo ni ahadi ya Rais John Magufuli aliyoitoa mara baada ya kuingia madarakani, ambapo kupitia bajeti ya wizara hiyo ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, ilitenga pia kiasi cha fedha kwa ajili ya ununuzi huo.
Kwa mujibu wa Waziri wake, Profesa Makame Mbarawa wakati akisoma makadirio ya mapato na matumizi ya mwaka 2016/17, serikali imejipanga kukamilisha ununuzi wa ndege mbili aina ya Bombardier Q400 kwa ajili ya ATCL ili kufufua safari za ndani za kampuni hiyo.
Hadi sasa ATCL ina ndege moja aina ya Bombadier Q300, hivyo ujio wa ndege hizo utaifanya kuwa na ndege nne zinazotoa huduma ya usafiri wa anga nchini.

New Force Dar - Songea Laua na Kujeruhi


Basi la New Force kutoka Dar es salaam kwenda Songea
limepata ajali baada ya kupinduka eneo la Kifanya kilomita kadhaa kutoka mkoani Njombe.
Ajali hiyo imetokea Septemba 19,2016 majira ya saa moja na dakika 40 usiku.
Inaelezwa kuwa watu 12 (wanawake 8,wanaume 4) wamepoteza maisha huku 9 wakijeruhiwa.
Abiria wa basi hilo wanasema basi lilikuwa katika mwendo kasi na kwamba lilinusurika kupinduka mara mbili na mara ya tatu ndipo likapinduka.
Kamanda wa polisi mkoa wa Njombe ACP Prudenciana Protas amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.

Abiria watozwa viingilio feki Kituo cha Ubungo

ABIRIA wa mabasi ya kwenda mikoani na nchi jirani katika Kituo cha Ubungo (UBT), wa- natozwa viingilio batili kiny- ume cha utaratibu.
Utaratibu unaojulikana abiria anapokuwa na tiketi hairuhisiwi kumtoza fedha za kiingilio ambayo ni Sh 300. Hata hivyo, hali ni tofauti kwani watu wote wamekuwa wakitozwa fedha za viingilio. Wakizungumza na MTANZANIA kwa nyakati tofauti, abiria hao walisema wameshangazwa na utaratibu huo,kwani siku zote wanaposafiri huingia katika kituo hicho kwa kutumia tiketi za mabasi wanayosafiria.
Mmoja wa abiria  hao Angela Yoredi aliyekuwa akisafiri kuelekea Dodoma na basi la ABC alisema ilimpasa kulipia kiingilio cha Sh 200, licha kuonesha tiketi yake mlangoni.
“Nashangaa imebidi nilipie Sh 200 wakati siku zote nikiwa na tiketi ya basi ninapita bila kulipia, waliniambia huo ni utaratibu mpya unaotumika kwa sasa,” alisema Angela.
Naye Mohamedi Issa ambaye alikuwa anasafiri na basi la Hood kwenda Morogoro alisema kwa sasa utaratibu wa kuingia katika kituo hicho haueleweki, kwani awali watu waliokuwa wanalipa ni wale waliokuwa wakiingia kituoni kwa ajili ya kupokea au kusindikiza abiria.
“Utaratibu wa humu sasa haueleweki pale mlangoni kuna abiria wanalipa Sh 200 lakini mimi nililipa Sh 300 in- gawa nilikuwa tayari na tiketi yangu ya basi,” alisema.
Akitoa ufafanuzi wa suala hilo, Ofisa Uzalishaji, Uratibu na Ushuru kituoni hapo, Novat Francis, alisema kitendo hicho ni kinyume cha sheria na uta- ratibu ambao umepangwa katika kituo hicho.

SERIKALI YAANZA KUTOA ELIMU KWA MAKONDA NA MADEREVA WANAOSAFIRISHA KEMIKALI

KATIKA kupunguza Madhara  ya Kemikali kwa wananchi, Serikali kupitia Wakala wa Mkemia Mkuu wameanza utoaji wa elimu kwa Madereva na Makondakta wa Magari ya usafirishaji wa bidhaa hizo ndani na je ya nchi.
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo jijini Dar es salaam Msimamizi wa Mifumo ya Ubora na Utafiti wa Kemikali katika Wakala wa Mkemia Mkuu wa Serikali BEN  MALYA, amesema kumekuwa na uelewa mdogo kwa Madereva na Makondakta juu namna ya kuepusha madhara ya kemikali pale ambapo magari ya kubeba bidhaa hiyo yanapopata ajali na kemikali kumwagika.

Kenya Airways yapunguza safari TZ kutoka 42-14 kwa wiki

Shirika la ndege la Kenya, Kenya Airways leo limeanza rasmi kupunguza safiri zake katika uwanja wa ndege wa Dar es Salaam kufuatia agizo la mamlaka ya anga ya Tanzania kuamuru shirika hilo kupunguza safari zake kutoka 42 kwa wiki hadi 14.
Serikali ya Tanzania inasema huo ndio mkataba wa tangu awali na kulaumu mamlaka ya anga nchini Kenya kwa kushindwa kuafikia maelewano na mamlaka ya Tanzania kuhusu jambo hilo.
Tayari baadhi ya wasafiri wanaotumia ndege za shirika hilo wameanza kuathirika kufuatia shirika hilo kufuta baadhi ya safari kutoka Dar es Salaam

MAAJABU: HILI NDO DARAJA LA MAJI DUNIANI...!!

 

Hili ni daraja linalopatikana nchini Ujerumani
Ujenzi wa daraja hili lenye maajabu yake duniani ulianza mnamo mwaka 1930 ambapo halikukamilika kufuatia vita kuu ya pili ya dunia hivyo ujenzi wake ulisimamishwa hadi mnamo mwaka 1997 mradi wa ujenzi uliendelezwa na lilifunguliwa rasmi mwaka 2003.
Daraja hili limekuwa likitumika na watu kusafirishia bidhaa kwa njia ya meli za mizigo lakini pia watu hutumia kuvuka upande mmoja kwenda mwingine na zaidi limekuwa kivutio kikubwa cha utalii
Daraja hili limepewa jina la Magdeburg Water Bridge
magdeburg-water-bridge2[3]magdeburg-water-bridge3[2]magdeburg-water-bridge4[2]magdeburg-water-bridge5[2]magdeburg-water-bridge6[13]

Shirika la ndege la Emirates kumwaga ajira kwa watanzania..!!

KATIKA  kutekeleza moja ya malengo ya Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Kimataifa, kupitia Ubalozi Mdogo wa Tanzania uliopo Nchini Dubai katika Falme za Kiarabu, umefanikiwa  kulishawishi Shirika la Ndege la Emirates  kuajiri Watanzania  kwenye Shirika hilo.
Shirika Limekubali kuajiri Watanzania katika kada mbalimbali, ambapo Maafisa wanaosimamia ajira kutoka Dubai wanatarajiwa kuja nchini Mwezi Machi mwaka huu kwa ajili ya kufanya usaili kwa Watanzania watakaoomba kazi kwenye Shirika hilo na kupata uteuzi wa awali.
Mkurugenzi Idara ya Mashariki ya Kati Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Simba Yahaya ameyasema hayo leo jijini Dar es salaam, alipokuwa akizungumza na wandishi wa habari ambapo amefafanua kuwa kupitia wandishi hao, Watanzania wenye sifa wataweza kufahamishwa juu ya fulsa za ajira katika Shirika hilo na kutuma maombi ya kazi.

Kama hukuona majambazi walivyoteka Mabasi Saba ya Abiria Arusha na Kupora Mali na Fedha, stori nzima iko hapa

Kundi la watu wanaosadikiwa kuwa majambazi, wameteka mabasi saba ya abiria yanayofanya safari zake kati ya Jiji la Arusha na Nairobi, Kenya na kupora mali na fedha ambavyo thamani yake haijafahamika.
Tukio hilo ambalo limethibitishwa na Jeshi la polisi, mkoani Arusha llitokea usiku wa kuamkia jana katika eneo la Mbuga Nyeupe, wilayani Longido Mkoa wa Arusha baada ya watu hao kuweka mawe barabarani na kuwamuru abiria wote kutemka mmoja baada ya mwingine, kulala chini na kuwapekua kila kitu walichokuwa nacho. DEREVA ALIYETEKWA ASIMULIA
Akisimulia mkasa huo, dereva wa basi la Perfect Trans, Joseph John, alisema kuwa watu hao waliokuwa na silaha za jadi yakiwamo mashoka, mapanga na sime, waliteka mabasi hayo majira ya saa 8 usiku.
“Hao jamaa walikuwa kama 50 hivi kwani waliteka magari yetu ambayo yalikuwa yamefuatana, wametuvua hadi viatu, saa yaani walipekua hadi wanawake waliamriwa kuvua nguo na kuporwa urembo wenye nakshi ya madini ya vito,” alisema John.
Alisema yeye alikuwa dereva wa kwanza kufika na basi katika eneo hilo na kuwa alipoona mawe yamepangwa kati kati ya barabara, aliamua kusimama na alipokuwa akijaribu kuyakwepa, alipigwa jiwe usoni hali iliyomfanya ashindwe kukimbia.
mabasi
“Hata wengine walikuwa hawajafunika nyuso zao, tukio lilidumu kwa dakika zaidi ya shirini, kila walipomaliza kupekua watu wa basi moja waliwaamuru warudi ndani ya gari,” alisimulia.
Dereva mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Jabir Athumani, alisema baadhi ya majambazi hayo yalikuwa yakiita majina ya baadhi ya watu na kuwaamuru kutoa fedha walizokuwa nazo.
“Tunaomba vyombo ulinzi na usalama vifuatilie tukio hili kwa umakini wa hali ya juu ili kuwanasa wahusika wa tukio hili,” alisema Jabir.
Aidha, alililitaka Jeshi la Polisi lirudishe magari ya doria katika barabara ya Arusha–Namanga ambayo yaliondolewa Aprili mwaka jana.
POLISI: TUTAZUNGUMZA LEO
Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuahidi kulitolea ufafanuzi leo.
“Hapa nipo katika majukumu mengine, sipo ofisini nitawapa taarifa za tukio lote Jumatatu (leo) mchana, naomba subiri nitafanya mkutano na vyombo vya habari na nitawapa maelezo ya tukio lote,” alisema Sabas.

Lori la Mafuta lapinduka Morogoro, likikwepa mtoto

Jeshi la polisi mkoa wa Morogoro limefanikiwa kudhibiti wananchi waliobeba madumu wakitaka kuiba mafuta baada ya lori la mafuta kuanguna katika eneo la Mikese mkoani Morogoro

Dereva wa lori Deogras John hilo akizungumzia tuki hilo la ajali amesema chanzo cha ajali alikua akijaribu kukwepa mtoto aliekua akivuka barabara ndipo gari ikapoteza mweleko na kupinduka mara kadhaa ambapo wananchi walijitokeza na madumu na kuanza kuiba mafuta. 
Nao wananchi wa eneo la Mikese katika hali iso ya kawaida wamelalamikia jeshi la polisi  kuwazuia kuiba mafuta na kueleza kuwa wamefanya kazi ya kumuokoa dereva kwa kumtoa kwenye gari na hivyo walipaswa kuchukua mafuta kama ujira wao

Magari kumi Ghali zaidi Duniani 2014-2015

1. Lamborghini Veneno $4,500,000
The Veneno gets you from 0 to 60 mph in a swift 2.8 seconds allowing you to hit a top speed of 221 mph. Only three cars are being made available every year. If you want to own this hyper-supercar, you will have to be placed on a waiting list along with other aficionados.

2. Lykan Hypersport $3,400,000
The Dubai based company W Motors are planning to make seven of these. The Lykan Hypersport is powered by a flat 6 twin-turbo engine, which produces 750 horsepower, and takes you from 0 to 60 in 2.8 seconds with an estimated top speed of 245 mph.
2013-W-Motors-Lykan-Hypersport-wheres-the-anvil A

3. Bugatti Veyron Super Sports $2,400,000.
 This is no longer the most expensive street legal production car available on the market today (the base Veyron costs $1,700,000). Capable of reaching 0-60 mph in 2.5 seconds, the Veyron is the fastest street legal car when tested again on July 10, 2010 with the 2010 Super Sport Version reaching a top speed of 267 mph (430 km/h). When competing against a Bugatti Veyron, you better be prepared!
Bugatti Veyron: Most Expensive Car in The World

4. Aston Martin One-77 $1,850,000
 The name "One-77" says it all: beauty and power in One, limited to 77 units. With 750 hp, it is able to go from 0 to 60 mph in 3.4 seconds with a maximum speed of 220 mph (354 km/h).
Very expensive and sexy car

4. Pagani Zonda Cinque Roadster $1,850,000.
 One of the most exotic cars out there is also one of the most expensive. It can go from 0-60 mph in 3.4 seconds with a top speed of 217 mph (349 km/h).

5. Zenvo ST1 $1,225,000
Able to reach 60 mph in 2.9 seconds and a top speed of 233 mph (375 km/h). The Zenvo ST1 is from a new Danish supercar company that will compete to be the best in speed and style. The ST1 is limited to 15 units and the company even promised "flying doctors" to keep your car running.

6. Lamborghini Reventon $1,600,000.
 The most powerful and the most expensive Lamborghini ever built takes third place on the list. It reaches 60 mph in 3.3 seconds from 0, to go with a top speed of 211 mph (339 km/h). Its rare (limited to 20) and slick design are reasons why it is expensive and costly to own. Lamborghini Reventon side view

6. Koenigsegg Agera R $1,600,000
 The Agera R goes from 0-60 mph in 2.8 seconds, reaching a maximum speed of 260 mph (418 km/h). It is capable of reaching 270 mph, but this supercar is electronically limited to 235 mph (378 km/h). You will need to sign a waiver, only then does the company unlock the speed limiter.

7. Maybach Landaulet $1,380,000
The Landaulet is the most expensive sedan on the market and it can go from 0-60 mph in 5.2 seconds. It is one the most luxurious cars ever made, this comes with a convertible roof that fully opens at the rear. This Maybach is made especially for CEOs and Executives who have their own personal driver.

8. McLaren P1 $1,350,000.
 McLaren announced that only 375 of the P1 will be made. Under the hood is a hybrid-modified 3.8 liter V8 twin-turbo engine. When combined with the electric motor, it is expected to produce 903 horsepower aided by a 7 speed dual clutch paddle shifter. Time trial estimates put the P1 to go from 0 to 60 in 2.7 seconds, while it is expected to have an electronically limited top speed of 217 mph.
2014-McLaren-P1-heat-test-drifting B

9. Pagani Huayra $1,300,000
Named after the "God of the winds" in Quechua, this Italian mid-engine comes with a 6.0 liter, V12 twin-turbo charged engine that produces 720 horsepower. It can reach from 0 to 60 mph in 3.0 seconds, and possibly reaching a top speed of 224 mph.
2013-Pagani-Huayra-studio-A

10. Hennessey Venom GT Spyder $1,100,000. 
What makes the 2013 Hennessey Venom GT Spyder is its price tag, a compelling 1.1 million dollars. There is no other convertible in the world today that can match-up with this car. Not to mention that it goes from 0-60 mph in 2.5 seconds.

TUME YA MIPANGO WATEMBELEA BANDARI YA BUKOBA


Displaying DSC08757.JPG
Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango wakiwasili kwenye Bandari ya Bukoba, walipofika kujionea bandari hiyo kongwe iliyopo kwenye fukwe za Ziwa Victoria, mkoani Kagera. Waliotangulia mbele ni Kiongozi wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (Wapili kulia). Wengine ni baadhi ya wajumbe wa msafara huo kutoka kushoto ni Bw. Omary Abdallah, Bibi Zena Hussein (Wapili kushoto) na Bw. Julius Edward (Kulia).
Displaying DSC08758.JPG
Madhari ya gati la Bandari ya Bukoba
Displaying DSC08764.JPG
Wajumbe wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango wakiwa kwenye ngazi za kupandia kwenye meli zinazotia nanga kwenye Bandari ya Bukoba.
Displaying DSC08771.JPG
Wajumbe wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango wakiwa kwenye Ofisi za Bandari ya Bukoba. Jengo la Ofisi hiyo limejengwa takriban miaka 70 iliyopita.  
Displaying DSC08773.JPG
Sehemu ya kupumzikia abiria ya Bandari ya Bukoba.
Displaying DSC08774.JPG
Wajumbe wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango wakiwa kwenye moja ya maghala ya kuhifadhia mizigo kwenye Bandari ya Bukoba.  
PICHA NA SAIDI MKABAKULI

KAGERA KUJIVUNIA UWANJA WA NDEGE WA KISASA

Na Saidi Mkabakuli, Kagera
Mkoa wa Kagera na maeneo ya jirani wataanza kujivunia uwanja wa ndege wa kisasa kufuatia kukamilika kwa Kiwanja cha Ndege cha Bukoba.
Akizungumza na Wakaguzi wa Miradi ya Maendeleo toka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Meneja Mradi wa Upanuzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kagera, Mhandisi Suleiman Athuman, amesema kwamba maendeleo ya ujenzi wa jengo la abiria la kiwanja hicho upo kwenye hali nzuri na mkandarasi atabidhi kazi hiyo mapema mwakani.
“Katika mwaka wa fedha wa 2013/14 kazi zilizopangwa ni ukarabati na upanuzi wa miundombinu ya kiwanja, ikijumuisha barabara ya kuruka na kutua ndege, maegesho ya ndege, barabara ya kiungio, kwa sasa ujenzi unaendelea vizuri na Mkandarasi atatukabidhi kazi mapema mwakani,” alisema Mhandisi Athuman.
Akitoa taarifa ya maendeleo ya ujenzi wa Kiwanja cha Bukoba, Mhandisi Mshauri wa ujenzi wa kiwanja hiko, Mhandisi Pius Gobolo amesema kuwa kazi za usimikaji wa mfumo wa taa za kuongozea ndege, ujenzi wa jengo jipya la abiria na uzio wa usalama zimeshakamilika kwa asilimia 80.
“Kama unavyojionea, sehemu kubwa ya kazi imekamilika, kwa makadirio ni zaidi ya asilimia 80 ya ujenzi wa kiwanja hiki imeshakamilika,” aliongeza   Mhandisi Gobolo.
Kwa mujibu wa mpangokazi wa ujenzi wa kiwanja hicho hadi kufikia mwezi Juni 2014, hatua iliyofikiwa ni pamoja na kukamilika kwa ukarabati wa barabara ya kuruka na kutua ndege, barabara ya kiungio na maegesho ya ndege kwa kiwango cha lami; na ujenzi wa jingo jipya la abiria kufikia hatua ya usimikaji wa paa na mifumo ya maji safi, maji taka na umeme; na kuendelea kwa ujenzi wa jengo la abiria na kituo cha umeme.
Naye, Kiongozi wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri amesema kuwa Serikali imeazimia kuendelea kuboresha miundombinu ya viwanja vya ndege hususan miradi iliyoibuliwa katika Programu ya Matokeo Makubwa Sasa.
“Kwa mujibu Programu ya Matokeo Makubwa Sasa, serikali kupitia Mamlaka ya Viwanja vya Ndege nchini ipo kwenye mkakati wa kuuendeleza viwanja vya ndege vyote ili viwe na kiwango kizuri kwa watumiaji wa viwanja hivyo,” alisema Bibi Mwanri.

Displaying DSC08652.JPG
Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango wakiwasili kwenye Kiwanja cha Ndege cha Kagera kujionea maendeleo ya Mradi wa Upanuzi wa Kiwanja hicho. Waliotangulia mbele ni Kiongozi wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (Kushoto), Meneja Mradi wa Upanuzi wa Kiwanja cha Ndege cha Bukoba, Mhandisi Suleiman Athuman (Katikati) na Meneja wa kiwanja hicho, Bw. Julius Mulungwana (Kulia).
Displaying DSC08668.JPG
Ujenzi unaendelea! Mafundi wakiendelea na ujenzi wa jengo la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kagera.
Displaying DSC08681.JPG
Displaying DSC08687.JPG
Mhandisi Mshauri wa ujenzi wa kiwanja hiko, Mhandisi Pius Gobolo akitoa maelezo ya namna ya kiwanja hicho kitakavyoonekana mara kitakapokamilika.
Displaying DSC08689.JPG
Pichani ni muonekano mpya wa Kiwanja cha Ndege cha Bukoba.
Displaying DSC08719.JPG
Wahandisi Pius Gobolo (kushoto), (Mhandisi Mshauri wa ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Bukoba) na Suleiman Athuman (watatu kulia), Meneja Mradi wa Upanuzi wa Kiwanja cha Ndege cha Bukoba wakitoa maelezo mara walipoingia kwenye sehemu ya abiria ya jengo jipya la kiwanja hicho.
Displaying DSC08729.JPG
Meneja wa kiwanja hicho, Bw. Julius Mulungwana (Kulia) akifafanua jambo kwa Kiongozi wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (Wapili kulia). Wanaoshuhudia ni Meneja Mradi wa Upanuzi wa Kiwanja cha Ndege cha Bukoba, Mhandisi Suleiman Athuman (Wapili kushoto) na Mhandisi Mshauri wa ujenzi wa kiwanja hiko, Mhandisi Pius Gobolo (Kushoto).
Displaying DSC08742.JPG
Hadi kuleeee.. Meneja wa kiwanja hicho, Bw. Julius Mulungwana (Mbele) akimuonesha Kiongozi wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (Kulia) sehemu inayopendekezwa kwa ajili ya upanuzi wa Kiwanja cha Ndege cha Bukoba.
Displaying DSC08745.JPG
imu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipangoimu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ikiendelea na kazi ya ukaguzi wa Kiwanja cha Ndege cha Bukoba.
PICHA NA SAIDI MKABAKULI

TIMU YA UKAGUZI WA MIRADI YA MAENDELEO KUTOKA OFISI YA RAIS, TUME YA MIPANGO YATEMBELEA MELI YA KIHISTORIA YA MV LIEMBA

Na Saidi Mkabakuli, Kigoma
Wakaguzi wa Miradi ya Maendeleo toka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango wamepata fursa adhimu ya kutembelea meli kongwe kupita zote nchini, MV Liemba iliyo kwenye Ziwa Tanganyika, mkoani Kigoma.
Wakizungumza mara walipofika katika meli hiyo baadhi ya wakaguzi hao hawakuficha bashasha waliyokuwa nayo mara baada ya kuingia ndani ya meli hiyo kongwe iliyo na umri zaidi ya miaka 100.
Mmoja wa wakaguzi hao Bibi Zena Hussein, alisema kuwa anajisikia furaha sana kuingia na kushuhudia mandhari ya meli hiyo ya kihistoria nchini Tanzania.
“Nimefurahi sana kufika leo hii kwenye meli hii yenye miaka zaidi ya 100, licha ya ukongwe wake bado inaonekana imara na yenye uwezo wa kufanya kazi miaka mingi zaidi,” alisema.
MV Liemba ni meli ya Kitanzania inayohudumia pwani za Ziwa Tanganyika. Ni chombo cha usafiri wa majini chenye umri mkubwa kuliko kingine chochote nchini na kipo tangu mwaka 1914. Meli hii kama zilivyo meli ningine inasukumwa na injini ya diseli na ina urefu wake ni mita 67, upana mita 10 na uzito wa tani 1500.
Kwa mujibu wa Nahodha wa meli hiyo, Kapteni Mathew Mwanjisi, meli hiyo ina uwezzo wa kubeba abiria 600 na tani za mizigo 200.
“Katika daraja la kwanza meli ina uwezo wa kubeba abiria 20, daraja la pili abiria 30 na daraja la tatu abiria 550,” alisema. 
Meli ya MV. Liemba inamilikiwa na Kampuni ya MSCL na kusajiliwa na Mamlaka ya Usafiri Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) kwa namba ya usajili KP/P001. Meli hiyo ilijengwa katika Bandari ya Kigoma mwaka 1913 na mjenzi kutoka Ujerumani kwa ajili ya usafirishaji wa mizigo na abiria.
Mv. Liemba ilitengenezwa nchini Ujerumani mwaka 1913 ikiwa ikiitwa kwa Kijerumani "Graf von Goetzen" kwenye kiwanda cha meli cha Meyer huko Papenburg.

Displaying DSC08206.JPG
 Displaying DSC08208.JPG
Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ikiwa ndani ya MV Liemba mara walipofika kujionea mandhari ya meli hiyo kongwe duniani.
Displaying DSC08212.JPG
Kiongozi wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (Kushoto) akisaini kitabu cha wageni ndani ya MV Liemba. Kulia ni Nahodha wa Meli hiyo, Kapteni Mathew Mwanjisi.
Displaying DSC08217.JPG
Displaying DSC08227.JPG
Nahodha wa MV Liemba, Kapteni Mathew Mwanjisi (Watatu kushoto) akitoa maelezo kwa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango.
Displaying DSC08237.JPG
Kiongozi wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (Wapili Kulia) akiiongoza Timu yake kusikiliza kwa umakini namna ya kusoma radar inayotumika ndani ya Meli ya MV Liemba. Anayewapa maelezo ni Nahodha wa Meli hiyo, Kapteni Mathew Mwanjisi.
Displaying DSC08242.JPG
Nahodha wa Meli ya MV Liemba, Kapteni Mathew Mwanjisi (Kulia) akitoa maelezo ya namna ya kutumia chombo cha kuokolea kwa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango. Wanaomsikiliza ni Kiongozi wa Timu hiyo, Bibi Florence Mwanri (Kushoto) na Kaimu Mkurugenzi wa Mipango na Ufuatiliaji (Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango), Bw. Omary Abdallah.
Displaying DSC08247.JPG
Mhandisi Mkuu wa Meli ya MV Liemba, Eng. Justine Joachim (Mwenye fulana nyeusi) akiwapa maelezo Wakaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango walipongia kujionea mitambo ya kuendeshea meli hiyo.
Displaying DSC08256.JPG
Kazi inaendelea! Watumishi wa Meli ya MV Liemba wakiendelea na kazi ya kushusha shehena ya mahindi kutoka kwenye meli hiyo.
PICHA NA SAIDI MKABAKULI