pagead2.googlesyndication.com pagead2.googlesyndication.com
Showing posts with label tragedy. Show all posts
Showing posts with label tragedy. Show all posts

The iPhone 7 is a Money Making Gimmick


The rumors can now be put to rest; Apple CEO Tim Cook revealed the latest Apple products on Sept. 8, where the company finally laid out the newest iPhone. Critics have talked about the iPhone 7 for months, speculating about what would be different. And finally, the public knows some rumors were true. For the first time in Apple iPhone history, their newest creation does not have a headphone jack.

Wait, what? I’m sure when you first heard this, and like me, you were confused and left with the burning question: How am I supposed to jam out to Yeezy now?
With the extinction of the popular headphone jack, Apple seems to be looking for ways to take more and more of our money. Sad thing is, we give it to them so willingly. Pre-orders have already begun for the iPhone 7, which starts out at $649 for the 32GB model, and stretches to an astounding $849 for a 256GB phone.
But the buck doesn’t stop there. Apple introduced a new product to replace the hassle of wired earbuds, making the lack of auxiliary port a non-issue. Wireless AirPods have been created for any future headphone needs, but they will not be available with the iPhone 7. The newest iPhone will come with EarPods and an adapter, allowing traditional headphones to connect through the lightning port.
At $159 a pair for new wireless headphones, techies are expected to spend almost $1,000 for the newest mobile gadgets. What have we come to, folks?
What in the world is Apple thinking charging consumers almost $200 for wireless earbuds? Not only is that outrageous but simply poor taste on Apple’s part. To charge an obscene amount of money to put something in your ears to simply listen to music is just pointless.
I don’t think Apple understands the demographic of those who purchase their products. Apple products appeal to a wide audience, one that is not limited to businessmen and women, groups such as college students.
We as college students have other necessities to pay for, leaving little money for trendy gadgets. If you own a car, you have a car payment, along with car insurance, gas and oil changes. If you live on your own, you have rent due every month, bills to pay and food to buy. We also have tuition to pay, or loans to pay off, making our budgets very tight.
Where does Apple get the idea that we have almost $200 to randomly drop on a pair of plastic wireless earbuds? Or even $600, $800 and $1,000, to buy their newest phone?
I know no matter what they produce and what they price it as, it will sell and Apple will make millions. But, what does this say about us as a society? Why should a measly headphone jack, or lack thereof, cause society to spend a month’s worth of rent on something that will be replaced by something bigger and better the following year or two.
Why get rid of the headphone jack in the first place? I was raised on the theory that, ‘if it isn’t broke, don’t fix it.’ What was wrong with the headphone jack and the wired earbuds? I was fine with untangling and unknotting my perfectly fine earbuds. If Apple really needed to create wireless earbuds, did they really need to get rid of the headphone jack?
No. They didn’t.
Let me know your thoughts on this my opinions

Majambazi waliohusika Mauaji Mbande Mabaroni

Pichani ni Nyumba inayosadikika kuhifadhi wahalifu
Watu saba wakiwemo watoto watatu wamekamatwa na polisi katika nyumba eneo la Vikindu Mashariki, Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani wakati polisi wakiendelea na oparesheni kufuatia mauaji ya askari polisi wanne eneo la Mbande wilaya ya Temeke mkoani Dar es Salaam.
Ripoti kutoka eneo la tukio zinasema askari bado ni wengi katika eneo la tukio wakiweka doria huku wananchi wakiwa wamesimama umbali wa takriban meta 50.
Kwa mujibu wa habari hizi milio ya risasi ilianza kusikika tangu Saa 8:20 usiku hadi saa 2 asubuhi.

Watanzania wengi wapo gerezani Afrika Kusini kwa ‘unga'


WAZIRI wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Augustine Mahiga amesema Watanzania wengi wanashikiliwa katika magereza ya Afrika Kusini kwa makosa ya kujishughulisha na biashara ya dawa za kulevya.
Alisema hayo wakati akifafanua suala la Watanzania wanaoishi nje ya nchi, hasa vijana na kusema wamekuwa wakijishughulisha na uuzaji dawa za kulevya badala ya kuwa raia wema.
Aliwataka kuacha kujishughulisha na mambo yanayoweza kuwaweka kwenye wakati mbaya na kutii sheria za nchi waliko.
Alisema Watanzania wengi waliopo Afrika Kusini wanafanya kazi ya kusafirisha dawa za kulevya na wengine wanasubiri ‘kuzamia meli’ mjini Durban.
Alisema suala hilo ni moja ya mambo ambayo yamekuwa yakijadiliwa na Serikali ya Afrika Kusini ambapo Tanzania imejulishwa tatizo hilo na Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya Afrika Kusini pamoja na Rais Jacob Zuma.
“Ni kweli lipo tatizo kubwa la Watanzania waliopo Afrika ya Kusini kujishughulisha na biashara ya dawa za kulevya. Serikali ya Afrika Kusini imetujulisha jambo hilo nasi tunalishughulikia kuiepusha nchi kuwa na uhusiano mbaya wa kidiplomasia na nchi nyingine.
Credit _ Habari Leo

Saudia yaendeleza mauaji ya raia nchini Yemen

Saudia yaendeleza mauaji ya raia nchini Yemen
Saudi Arabia imefanya mashambulizi mapya ya anga nchini Yemen na kupiga maeneo kadhaa ya nchi hiyo maskini ukiwemo mji mkuu, San'aa. Ripoti zimeeleza kuwa, ndege za kivita za Saudi Arabia zimeushambulia mji wa San'aa na kuwauwa watu 23 wakiwemo wanawake tisa na watoto wawili. Ndege za kivita za Saudia pia zimeushambulia mji wa Haradh katika mkoa wa kaskazini mwa Yemen wa Hajjar karibu na mpaka wa nchi hiyo na Saudi Arabia. Ndege hizo pia zimefanya mashambulizi sita katika wilaya ya Jidan katika mkoa wa Ma'rib katikati mwa Yemen. Ripoti zimeeleza pia kuwa magari matatu ya raia yameshambuliwa na ndege za kivita za Saudia katika wilaya ya Hazm katika mkoa wa al Jawf huko kaskazini magharibi mwa Yemen.
Wakati huo huo Maelfu ya raia wa Yemen wamefanya maandamano makubwa leo mjini San'aa na katika miji mingine ya nchi hiyo wakipinga mashambulizi ya kinyama yanayoendelea kufanywa na jeshi la Saudi Arabia na washirika wake dhidi ya watu wa nchi hiyo.
Maelfu ya raia wasio na hatia wa Yemen wameuawa na malaki ya wengine kuwa wakimbizi katokana na mashambulizi hayo ya Saudia

Hizi ndo picha za tukio la majambazi kuua Askari na kupora bunduki kituo cha Polisi Ikwiriri

Samahani kwa picha utakazoziona:
Askari wawili wa Jeshi la Polisi katika Kituo cha Ikwiriri wilayani Rufiji mkoani Pwani, wameuawa baada ya kushambuliwa kwa silaha na majambazi, waliovamia kituo hicho na kuiba silaha baada ya kufanikisha mauaji.
  afande
Kutokana na tukio hilo, Jeshi la Polisi liko katika msako mkali, huku Mkuu wa jeshi hilo, IGP, Ernest Mangu akitangaza donge nono la Sh milioni 20 kwa watakaofanikisha kukamatwa kwa wahusika wa tukio hilo na silaha.
 
Akizungumza na waandishi wa habari kwa njia ya simu kutoka eneo la tukio, Ikwiriri, Kamanda wa Polisi mkoani Pwani, Ulrich Matei alisema majambazi hao walitumia silaha kuwaua askari hao.
 
Kamanda Matei alisema kuwa tukio hilo lilitokea majira ya saa 8 usiku katika kituo hicho cha Polisi cha Ikwiriri. Aliwataja askari waliokufa kuwa ni mwenye namba E 8732 Koplo Edgar Milinga na WP 5558 Konstebo Judith Timothy.
 
Alisema licha ya kufanya mauaji hayo, pia majambazi hayo yalipora silaha tano za moto aina mbalimbali, zikiwemo SMG 2, SAR 3 na risasi 60. Pia, walichukua mabomu mawili ya machozi.
 
Kamanda alisema kuwa pia watu hao, waliharibu kwa kulipiga risasi gari la Polisi la kituo hicho lenye namba za usajili PT 1965.
 
Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, Advera Bulimba alisema tukio hilo la kusikitisha, halitapita hivi hivi, bali jeshi limeelekeza nguvu zake huko kuhakikisha wahusika wanakamatwa.
 
Alisema tayari Mkuu wa Jeshi ametangaza dau la Sh milioni 20. Pia, alisema katika kuongeza kasi ya msako, Kamishna wa Operesheni na Mafunzo, Paul Chagonja akiwa na timu ya makachero, yuko eneo la tukio kuhakikisha wahusika, kokote waliko, wanasakwa na kutiwa mbaroni.
 
“Hili ni sawa na tukio la kigaidi, Jeshi la Polisi litakabiliana na wahusika kokote waliko, lazima wakamatwe. Kikubwa tunaomba ushirikiano wa wananchi, tunaamini wengi ni raia wema na watalisaidia jeshi kufanikisha jukumu hilo la kukomesha uhalifu nchini,” alisema Advera.
 
Aliwataka wananchi kuelewa Jeshi la Polisi liko imara, hivyo wasiwe na hofu yoyote juu ya tukio hilo. Alisisitiza kuwa wahusika wote watadhibitiwa na kushikishwa adabu

Viongozi wa kanisa la Baptist wapigwa na kutekwa nyara Guinea

VIONGOZI watatu wa kanisa la Baptist nchini Guinea wamepigwa na kisha kutekwa nyara baada ya wenyeji kudhani kwamba  walikuwa  maafisa wanaohamasisha jamii dhidi ya ugonjwa wa Ebola .
Viongozi hao walikuwa wametembelea kijiji cha kabac eneo la forecariah wakilenga kufukiza dawa ya wadudu kwenye kuta za vyoo vya umma  ikiwa ni sehemu pia ya kujipatia  huduma ya maji .
Taarifa zimesema kuwa wanakijiji hao walipowaona waliwashuku kuwa wanataka kueneza ugonjwa wa ebola  katika eneo hilo .

Maaskari kadhaa wauawa na silaha kuchukuliwa katika kituo cha Polisi cha Ikwiriri Wilayani Rufiji




Kituo cha Ikwiriri,Wilayani Rufiji kilishambuliwa usiku wa kuamkia leo na watu waliojihami na silaha na kusababisha vifo vya Maaskari wawili na wengine wakijeruhiwa vibaya kufuatia tukio hilo.

Habari kutoka Wilayani Rufiji mkoa wa Pwani nchini Tanzania zinaarifu kuwa watu waliokuwa na silaha wamefanya shambulio kubwa usiku wa kuamkia leo na kusababisha hasara kwa Maaskari waliokuwa zamu kwenye kituo hicho.


Hata hivyo washambuliaji walichukua silaha mbalimbili zilizohifadhiwa katika kituo hicho,wakaazi wanasema walisiki milio ya risasi zikirindima hovyo na kuwasababishia khofu.


Kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani Urich Matei amethibitisha kutokea shambulio hilo na kusema kuwa shambulio hilo limetokea saa 8:00 usiku na kusababisha vifo vya Maaskari Polisi wawili na silaha kadhaa kuchukuliwa ambazo zilihifadhiwa kwenye kituo hicho.

Ni shambulio la kwanza kufanyika nchini Tanzania tangu kwanza kwa mwaka huu 2015,Mashambulio mengine kama haya pia yalifanyika kwenye vituo vya Polisi Kimanzichana,Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani,na Wilaya ya Bukombe mkoani Geita nchini Tanzania.

Serikali kibaraka nchini Tanzania inawashikilia mamia ya Waislaam na kuendelea kuwapa adhabu yalio na kinyume na haki za kibinaadam kwa kisingizio cha tuhumu za Ugaidi na wengine ikiwaua ambapo tukio la mwisho kikosi cha kupambana na Ugaidi nchini humo iliwaua vijana kadhaa katika miji ya Arusha,Morogoro na Zanzibaar.

Mapigano makali mji wa San'aa; wanamgambo wa Kishia wakaribia kuiteka Ikulu ya Yemen.

Habari kutoka nchini Yemen zinaeleza kuwa mapigano makali yamepamba moto katika mji mkuu wa nchi hiyo wakati ambapo wanamgambo wa Kishia wa Huthi wakijaribu kuuteka Ikulu ya nchi hiyo.

Mapigano hayo yalikuja wakati ambapo wanamgmbo wa Huthi walipofanya mashambulio ya kupangwa dhidi ya kikosi cha Haraasul Jamhuri wanaolinda Ikulu ya Rais wa nchi hiyo.

Waandishi wa habari waliripoti jana kuwa makali ya mapigano yaliendelea kusini mwa mji wa San'aan na pembezoni mwa Majengo ya Kasri ya Ikulu wa Rais Abdi Rabih Hadi Mansuri kiongozi wa Utawala Kibaraka wa Yemen.

Habari zaidi zinaeleza kuwa wanamgambo wa Kishia wa Yemen wanajaribu kuuchukua Ikulu ya nchi hiyo siku mbili zilizopita walimteka Mkurugenzi wa Ikulu,na inaaminika wanasonga pole pole kuelekea Ikulu.

Mwezi september mwaka jana wanamgambo hao walio mawakala wa Iran waliutwaa mji wa San'aa na maeneo mengi ya miji muhimu nchini Yemen.

Kama hukuona majambazi walivyoteka Mabasi Saba ya Abiria Arusha na Kupora Mali na Fedha, stori nzima iko hapa

Kundi la watu wanaosadikiwa kuwa majambazi, wameteka mabasi saba ya abiria yanayofanya safari zake kati ya Jiji la Arusha na Nairobi, Kenya na kupora mali na fedha ambavyo thamani yake haijafahamika.
Tukio hilo ambalo limethibitishwa na Jeshi la polisi, mkoani Arusha llitokea usiku wa kuamkia jana katika eneo la Mbuga Nyeupe, wilayani Longido Mkoa wa Arusha baada ya watu hao kuweka mawe barabarani na kuwamuru abiria wote kutemka mmoja baada ya mwingine, kulala chini na kuwapekua kila kitu walichokuwa nacho. DEREVA ALIYETEKWA ASIMULIA
Akisimulia mkasa huo, dereva wa basi la Perfect Trans, Joseph John, alisema kuwa watu hao waliokuwa na silaha za jadi yakiwamo mashoka, mapanga na sime, waliteka mabasi hayo majira ya saa 8 usiku.
“Hao jamaa walikuwa kama 50 hivi kwani waliteka magari yetu ambayo yalikuwa yamefuatana, wametuvua hadi viatu, saa yaani walipekua hadi wanawake waliamriwa kuvua nguo na kuporwa urembo wenye nakshi ya madini ya vito,” alisema John.
Alisema yeye alikuwa dereva wa kwanza kufika na basi katika eneo hilo na kuwa alipoona mawe yamepangwa kati kati ya barabara, aliamua kusimama na alipokuwa akijaribu kuyakwepa, alipigwa jiwe usoni hali iliyomfanya ashindwe kukimbia.
mabasi
“Hata wengine walikuwa hawajafunika nyuso zao, tukio lilidumu kwa dakika zaidi ya shirini, kila walipomaliza kupekua watu wa basi moja waliwaamuru warudi ndani ya gari,” alisimulia.
Dereva mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Jabir Athumani, alisema baadhi ya majambazi hayo yalikuwa yakiita majina ya baadhi ya watu na kuwaamuru kutoa fedha walizokuwa nazo.
“Tunaomba vyombo ulinzi na usalama vifuatilie tukio hili kwa umakini wa hali ya juu ili kuwanasa wahusika wa tukio hili,” alisema Jabir.
Aidha, alililitaka Jeshi la Polisi lirudishe magari ya doria katika barabara ya Arusha–Namanga ambayo yaliondolewa Aprili mwaka jana.
POLISI: TUTAZUNGUMZA LEO
Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuahidi kulitolea ufafanuzi leo.
“Hapa nipo katika majukumu mengine, sipo ofisini nitawapa taarifa za tukio lote Jumatatu (leo) mchana, naomba subiri nitafanya mkutano na vyombo vya habari na nitawapa maelezo ya tukio lote,” alisema Sabas.

Boko Haram wavamia Cameroon, watu 70 washukiwa kutekwa..!

Askari jeshi wanaodhaniwa kuwa wapiganaji wa kundi haramu Boko Haram wameteka watu zaidi ya 60 katika nchi jirani ya Cameroon imethibitika.
Inasemekana miongoni mwa mateka wengi wao ni watoto waliokamtwa mpakani mwa nchi mbili hizo.Na inaarifiwa kuwa watu kadhaa waliuawa wakati wa utekelezaji wa tukio hilo.
Boko Haram siku za hivi karibuni zimekamata udhibiti wa miji kadhaa na vijiji upande wa kaskazini Mashariki mwa Nigeria, na sasa wameanza kuwa tishio kwa nchi jirani wanazopakana na Nigeria .Katika shambulio hilo la siku ya Jumapili askari hao walivamia vijiji viwili vilivyoko eneo la Tourou .
Katika uvamizi huo nyumba kadhaa zilichomwa moto na idadi ya mateka ni themanini kati yao watu wazima ni thelathini,na watoto wapatao hamsini na walielekea upande wa Kaskazini mwa Cameroon .
Kundi hilo limepigana vita takribani miaka sita sasa, wakijaribu kuusimika utawala wa dola ya kiislam nchini humo.

Marekani yapiga marufuku adhana chuo kikuu Duke

Marekani yapiga marufuku adhana chuo kikuu Duke
Katika mwendelezo wa chuki dhidi ya dini na matukufu ya Kiislamu, Marekani imepiga marufuku adhana katika Chuo Kikuu cha Duke nchini humo. Chuo Kikuu cha Duke ambacho hivi karibuni kilikuwa kimetoa ruhusa kwa Waislamu wa chuo hicho kuadhini, kimepiga tena marufuku suala hilo. Wiki iliyopita, viongozi wa chuo hicho  kilichopo katika jimbo la Carolina kaskazini walitoa taarifa rasmi iliyoruhusu adhana kupitia mnara wa kanisa shuleni hapo. Awali Michael Schoenfeld, Naibu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Duke alinukuliwa akisema kuwa, wanafunzi wa Kiislamu wamekuwa na mchango mkubwa katika ustawi wa chuo na kwamba bodi ya shule inakubali watekeleze ibada zao shuleni hapo. Hata hivyo ghafla viongozi wa chuo hicho wamepiga marufuku adhana bila kutolewa sababu maalumu. Baadhi wanamtaja Franklin Graham, kasisi wa Kimarekani kuwa chanzo cha marufuku hiyo, hasa kwa kuzingatia kuwa hivi karibuni alitishia kukata misaada yake kwa chuo hicho  ikiwa Waislamu wataruhusiwa kuadhini chuoni hapo.

Al-Shabaab 'yasambaratika' baada ya mashambulizi ya anga, uasi

Wanajeshi wa Somalia wakiangalia miili ya wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa al-Shabaab waliouawa wakati wa mapigano ya kufyatuliana risasi mjini Mogadishu hapo tarehe 26 Disemba, 2014, siku moja baada ya wanamgambo kushambulia makao makuu ya Kikosi cha Kulinda Amani cha Umoja wa Afrika nchini Somalia. AMISOM ilisema kwamba wanajeshi wake walirejesha udhibiti wa kambi hiyo mjini Mogadishu baada ya mapigano ya bunduki kuua washambulizi watano na wengine watatu kukamatwa.  [Na Mohamed Abdiwahab/AFP]Huku viongozi wa al-Shabaab wakiuawa katika mashambulizi ya anga yaliyolengwa na wapiganaji wake kuasi kwa idadi kubwa, serikali ya Somalia na washirika wake wana fursa ya kutumia faida ya hali dhaifu ya kundi hilo, wachambuzi wanasema.
  • Wanajeshi wa Somalia wakiangalia miili ya wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa al-Shabaab waliouawa wakati wa mapigano ya kufyatuliana risasi mjini Mogadishu hapo tarehe 26 Disemba, 2014, siku moja baada ya wanamgambo kushambulia makao makuu ya Kikosi cha Kulinda Amani cha Umoja wa Afrika nchini Somalia. AMISOM ilisema kwamba wanajeshi wake walirejesha udhibiti wa kambi hiyo mjini Mogadishu baada ya mapigano ya bunduki kuua washambulizi watano na wengine watatu kukamatwa.

  • "Hasara ambayo al-Shabaab imekuwa ikipata kwa mfululizo katika miaka miwili iliyopita inaonekana kuwa ni tishio kwa uwepo wa kundi hilo," alisema Abdirahim Isse Addow, mkurugenzi wa Redio Mogadishu inayoendeshwa na serikali na msemaji wa zamani wa Umoja wa Mahakama za Kiislamu, umoja ambalo al-Shabaab ilijitenga nalo.
    "Ishara za kutengana kwa al-Shabaab ni dhahiri sana," Addow aliiambia Sabahi. "Hakuna kikundi kinaweza kuendelea kuwepo wakati kinapoteza uungwji mkono na jamii ambayo ipo ndani yake."
    Kutokana na matokeo ya mashambulizi ya Seriklai ya Somalia na Kikosi cha Kulinda Amani cha Umoja wa Afrika Somalia, (AMISOM), al-Shabaab imepoteza mapato ambayo ilikuwa ikipata kutoka miji muhimu kama vile Barawe, Kismayu, Bulo Burde na El Bur, alisema.
    Aidha, alisema, migogoro ya ndani ya al-Shabaab, ambayo imeikumba kikundi katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita, imekuwa na athari za kudumu katika kuvunja uongozi wa kikundi hicho.
    Migawanyiko ndani ya kikundi hicho ilikuwa mikubwa sana ambayo hatimaye ilipelekea kiongozi wa zamani wa al-Shabaab Ahmed Abdi Godane kuandaa mauaji ya makamanda wengi wa zamani, ikiwa ni pamoja na mwanzilishi mwenza wa al-Shabaab Ibrahim Meeaad al-Afghani, mpiganaji jihadi mzaliwa wa Marekani Abu Mansour al-Amriki na Maalim Burhan, Addow alisema.
    "Baada ya hapo, watu wengine wengi ambao waloikuwa sehemu ya kikundi hicho walikimbia, wakiwemo Mukhtar Robow, Hassan Dahir [Aweys] na Zakariya [Ismail Ahmed Hersi], ambaye hatimaye alijisalimisha kwa serikali," alisema.
    Kikundi hicho kamwe hakikurejea kuotka hali ya kuvunjika katika uongozi wake, ambao sasa umekuwa ukimalizwa kwa mashambulizi ya anga yanayowaua viongozi waliobakia, Addow alisema.
    Katika mfano wa karibuni zaidi wa shambulio la anga lililofanikiwa dhidi ya uongozi wa al-Shabaab, mkuu wa upelelezi wa kikundi hicho Abdinasir Hassan Barakobe, ambaye majina yake mengine yalikuwa ni pamoja na Abdishakur na Tahlil, aliuawa tarehe 29 Disemba karibu na Saakow, kwenye Mkoa wa Jubba ya Kati nchini Somalia.
    Kifo chake kilikuja siku mbili baada ya kujisalimisha kwa mkuu wa upelelezi wa al-Shabaab Hersi kwa mamlaka za Somalia.
    Kabla ya kuuawa, mengi yalikuwa hayajulikani kuhusu Barakobe, ambaye alikuwa katika umri wa miaka 30 na alizaliwa katika familia maarufu huko wilaya ya Bondhere mjini Mogadishu. Alikuwa mmoja wa maafisa wa Umoja wa Mahakama za Kiislam na baadaye alijiunga al-Shabaab mwaka 2007
    Barakobe alikuwa akiaminika kuwa alikuwa karibu sana na Godane na baada ya kifo chake iliibuka kuwa yeye ndiye aliyekuwa na dhamana wa kitengo cha upelelezi cha Amniyat

    Fursa ya kuiangamiza al-Shabaab

    "Serikali ya Somalia ina fursa kubwa ya kuliangamiza kundi hili kwa msaada wa washirika wake," alisema Abdirisaq Mohamed Qeylow, ambaye alikuwa msemaji wa Muungano wa Mahakama za Kiislamu kabla ya kujiunga na serikali ya Somalia na kuwa msemaji wa Wizara ya Habari chini ya Rais Sheikh Sharif Sheikh Ahmed wa Serikali ya Mpito ya Shirikisho.
    "Kipindi cha msamaha kinapaswa kuongezwa na fursa zilizotolewa kwa watu ambao hawajafanya makosa makubwa, kama vile vijana, lazima ziongezwe kama vile elimu, kazi na kuwahakikishia usalama wao kama njia ya kuwavutia vijana ambao bado wamo kwenye kundi hilo," aliiambia Sabahi.
    Hatima ya wanachama wa al-Shabaab ni katika ya vigawe vitatu, kwa mujibu wa Qeylow.
    "Kwanza ni viongozi wakuu wa kundi hilo, ambao baadhi yao wamefanya makosa makubwa dhidi ya watu wa Somalia," alisema. "Haitawezekana kwao kujificha ndani ya jamii na serikali ya Somalia haiwezi kufanya maamuzi juu yao peke yake ikiwa watajisalimisha kwa sababu wamefanya makosa makubwa dhidi ya dunia. Hivyo, watajaribu kupigana hadi wauawe."
    "Kuna kundi la pili. Hawa ni watu ambao hawafahamiki sana na watu, lakini wana nguvu kwenye kundi hilo. Hao ni watu walio na fursa ya kujisalimisha na kujitenga mbali na shughuli walizokuwa wakijihusisha nazo wakiwa sehemu ya al-Shabaab," alisema. "Kundi la tatu ni wanachama vijana wa al-Shabaab ambao wanabeba silaha. Hao hujisalimisha kila siku na na kurekebishwa kitabia."
    "Kundi hili halitaweza kuendelea kubakia kama mambo yanakwenda kama hivi," Qeylow aliongeza.
    Ugumu wa al-Shabaab katika kuwabakisha wapiganaji wake wa kigeni na kuwavutia wapya pia unaonesha matatizo ya kundi hilo.
    "Katika siku za karibuni kumekuwa hakuna habari juu ya wapiganaji wa kigeni wanaopigana upande wa al-Shabaab. Nadhani wengi wao wameondoka nchini na wamejiunga na mapigano yanayoendelea kwenye nchi za Kiarabu kama Libya, Yemen na Syria," alisema Qeylow. "Jambo hilo limedhoofisha nguvu za al-Shabaab, ambayo mwanzoni ilikuwa inaungwa mkono kiitikadi na kifedha na al-Qaida."
    "Inawezekana kwamba baada ya kuuawa kwa Fazul Abdullah Mohammed, ambaye alikuwa mkuu wa al-Qaida kwenye eneo la Afrika Mashariki na aliyekufa kwenye mtego wa Godane, na barua ya malalamiko iliyoandikwa na Ibrahim al-Afghani, ambaye pia aliuawa na Godane, kulishusha uungaji mkono wa al-Qaida na makundi mengine (kwa al-Shabaab)," alisema.

    Kupambana na itikadi ya al-Shabaab

    Wimbi la kushindwa lililoikumba al-Shabaab katika siku za karibuni limeufanya uongozi wake kusambaratika na kundi hilo kudhoofika, alisema mchambuzi wa masuala ya kisiasa Hassan Sheikh Ali, lakini itikadi kali ambalo kundi hilo linaisambaza itaendelea nchini Somalia kwa miaka mingi ijayo.
    "Al-Shabaab imekuwa ikienda chini kwa miaka mitatu iliyopita, lakini mauaji ya hivi karibuni ya viongozi wao wa juu yatatumika kwa kuharibu [kudumu] uwezo wa kijeshi wa kundi, nguvu na ari hivi karibuni," Ali aliiambia Sabahi. "Lakini kama itikadi, al-Shabaab itakuwa hapa kwa muda mrefu na itabi8di ipigwe vita kwa itikadi nyingine."
    "Al-Shabaab inaumia pia kwa sababu wapiganaji wa kigeni waliokuwa wakija hapa kwa ajili ya jihadi sasa wanakwenda Syria na Iraq," alisema. "Kwa hivyo, serikali ya shirikisho ya Somalia, serikali za mikoa na majimbo, na jamii ya kimataifa lazima zichukue fursa kwa hali ya kudhoofika ya al-Shabaab iliyonayo sasa."
    "Ili kufanya hivyo, serikali lazima iepuke migogoro ya kisiasa ambayo inaudhoofisha uwezo wake wa kufanya kazi," alisema.
    Kundi kama al-Shabaab linaweza tu kudumu ikiwa lina uongozi imara, alisema Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Vijana wa Somalia, Mukhtar Haji Kastaro. "Lakini [msingi wa] al-Shabaab umeharibiwa. Katika miezi michache ya hivi karibuni, viongozi wake wengi wakuu wameuawa na serikali isipoteze fursa hii," aliiambia Sabahi.
    "Baadhi ya hatua ambazo serikali na AMISOM wanapaswa kuzichukuwa ni pamoja na kuchukuwa udhibiti wa haraka wa wilaya zilizo chini ya al-Shabaab ili kutowapa fursa ya kujikusanya tena, kujiingiza kwenye mazungumzo na viongozi wa al-Shabaab wenye msimamo wa wastani na kuendelea kuwaandama [kwa kuwauwa] wale wachache wenye siasa kali waliobakia kwenye kundi hilo."
    "Hilo likifanyika, al-Shabaab inaweza kuharibiwa moja kwa moja ndani ya kipindi cha miezi 12 ijayo kwani inapumua upumzi wake wa mwisho," alisema.

    Mafuriko yawaua watu 170 Malawi

    Takriban watu 170 wanaripotiwa kuaga dunia kwenye mafuriko ambayo yameikumba Malawi kwa karibu mwezi mmoja sasa.
    Watu wengine 100,000 wamelazimika kuhama makwao.
    Mapema wiki hii rais Peter Mutharika alitangaza thuluthi moja ya nchi hiyo kuwa katika hali ya hatari na kuomba msaada wa kimataifa.
    Zaidi ya watu wengine 50,000 wamehama makwao katika nchi jirani ya Msumbuji kutokana na mafuriko hayo.

    IS wafungua kambi za mafunzo Libya


    Wapiganaji wa kundi la Islamic State wafungua kambi za mafunzo Libya
    Wapiganaji wa kundi la Islamic State wameanzisha kambi za mafunzo mashariki mwa Libya, amesema mkuu wa kamandi ya Marekani ya masuala ya Afrika.
    Jenerali David Rodriguez amesema kuna mamia ya wapiganaji wa IS wanaopata mafunzo ya kijeshi kwenye kambi zake nchini Libya. Amesema kambi hizo zipo katika hatua za mwanoz kabisa, lakini Marekani imekuwa ikiyafuatilia kwa karibu kuona zinavyoendelezwa.
    Libya imekuwa katika mgogoro tangu kuangushwa kwa utawala wa Muammar Gaddafi mwaka 2011, ambapo makabila mbalimbali, wanamgambo na makundi ya kisiasa, wote wakipigania madaraka.
    Makundi mbalimbali ya Kiislam yanawania madaraka mashariki mwa Libya, huku baadhi yakitangaza kuwa na ushirikiano la kundi la Islamic State, IS.
    Akizungumza mjini Washington Jumatano, Jenerali Rodriguez bado haijafahamika ukaribu uliopo kati ya watu wanaopata mafunzo hayo na kundi la IS.
    "Kikubwa ni watu wanaokuja kupata mafunzo na msaada wa vifaa kwa ajili ya kambi za mafunzo kwa sasa," amesema. "kwa sasa mafunzo hayo bado ni ya hatua ya chini sana na tunafuatilia kuona namna hali inavyokwenda."
    Waandishi wa habari wanasema katika kipindi cha mapinduzi yaliyomwondoa madarakani Gaddafi, wapiganaji wengi waasi waliondoka nchini humo kwenda kujiunga na vikundi vya wapiganaji nchini Syria na baadhi yao wanaaminika kuwa wamerejea nyumbani(Libya).
    Serikali iliyochaguliwa imepoteza miji mikuu mitatu ya Libya huku kukiwa na mgogoro wa kisiasa.
    Benghazi, mji wa pili kwa ukubwa nchini Libya, uko mikononi mwa wapiganaji wa Kiislam, na bunge linalotambuliwa kimataifa kwa sasa linaendesha vikao vyake katika mji ulioko pwani ya Tobruk mashariki mwa nchi hiyo.
    Marekani imekuwa ikiongoza washirika wa kimataifa kufanya mashambulio ya anga dhidi ya IS nchini Iraq na Syria katika miezi ya karibuni.

    Mlipuko mkubwa wakumba Mogadishu

    Mlipuko mkubwa umetokea katika mji wa Mogadishu nchini Somalia karibu na uwanja wa ndege.

    Duru zimearifu kuwa mlipuko huo huenda umesababishwa na mtu aliyejitolea muhanga aliyejilipua ndani ya gari.
    Kundi la wapiganaji wa kiislamu la Al- Shaabab mara kwa mara hutumia milipuko ya magari, lakini kufikia sasa halijakiri kuhusika na mlipuko huo.
    Haijajulikana ni watu wangapi wameuwawa.

    Farc wagoma kumuachia Jenerali Colombia

    Waasi wa nchini Colombia, Farc wamesema wataahirisha zoezi la kuachiwa kwa kiongozi wa juu wa jeshi, na watu wengine wanaoshikiliwa mateka, kwa sababu ya uwepo wa wanajeshi wa serikali katika eneo wanaposhikiliwa mateka hao.
    Katika taarifa ya waasi, wamedai kuwa kumekuwa na wanajeshi wengine katika jimbo la Choco.
    Serikali iliahirisha kufanyika kwa mazungumzo ya amani yaliyokuwa yakifanyika kati yake na waasi nchini Cuba baada ya kutekwa nyara kwa Jenerali Alzate.
    Waasi walisema wanampango wa kuwaachia mateka siku ya jumanne.
    Jenerali Alzate alitekwa nyara pamoja na Wanajeshi wawili tarehe 16 mwezi huu.
    Siku ya Jumamosi, Rais wa Colombia Juan Manuel Santos alitangaza kuwa Waasi wa Farc wameridhia kuwaachia mateka hao wiki hii bila kutaja tarehe.
    Lakini hivi sasa waasi wamesema hawawezi kufanya kama walivyoahidi kutokana na yanayoendelea sasa.
    Ruben Dario Alzate ni jenerali wa kwanza nchini Colombia kutekwa katika mgogoro uliodumu kwa kipindi cha miaka 50.
    Timu ya wawakilishi wa Farc kwenye mazungumzo ya amani imesema kuwa wanajeshi wamefika katika eneo wanaposhikiliwa mateka hali inayosababisha kuahirishwa kwa zoezi hilo mpaka pale hali itakapokuwa shwari.
    Inakisiwa kuwa watu 220,000 wamepoteza maisha tangu ulipotokea mzozo nchini Colombia.

    Kanali ahukumiwa kunyongwa,Congo Dr

    Mahakama ya kijeshi Mashariki mwa Jamuhuri ya Demokrasi ya Congo imemhukumu kifo Kanali Birocho Nzanzu baada ya kubainika na makosa ya kutaka kumuua afisa wa jeshi la nchi hiyo aliyekuwa mstari wa mbele kutokomeza wapiganaji wa M23.
    Afisa anayedaiwa kupangiwa njama za kuuawa ni Mamadou Ndala mabaye kwa kiasi kikubwa aliamini katika vita dhidi ya kundi hilo la wapiganaji na ambaye aliuawa mwezi januari mwaka huu. Hata hivyo hukumu hiyo imetolewa kwa watuhumiwa nane ambapo kati ya hao mmoja ndiye Kanali Ndala aliyehukumiwa kifo. Mahakama imebainisha kuwa Kanali Nzanzu amekuwa akitumiwa na waasi wa ADF kutoka Uganda kuandaa maujaji.

    Madudu zaidi meno ya tembo

    Balozi wa China, Lu Youqing akizungumza, jana mjini Arusha wakati wa Mkutano wa Kimataifa wa Kudhibiti Ujangili. Wengine ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu (katikati) na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, James Lembeli Picha na Filbert Rweyemamu 

    Dar es Salaam. Wakati maofisa wa Serikali za Tanzania na China wakipuuza tuhuma zinazohusisha ziara ya Rais wa China, Xi Jinping na utoroshaji wa meno ya tembo, ripoti hiyo imeanika madudu mengi ikionyesha jinsi nyara hizo zinavyotoroshwa nchini.
    Juzi taasisi iitwayo Environmental Investigation Agency (Wakala wa Uchunguzi wa Mazingira– EIA) ilitoa hadharani ripoti ambayo inataja maofisa na wanausalama wa China kwamba walitumia fursa ya kidiplomasia kusafirisha meno ya tembo kwa ndege ya Rais Jinping ambaye alitembelea Tanzania Machi 2013.
    Ikulu ya Dar es Salaam na Ofisi ya Mambo ya Nje ya China kwa nyakati tofauti zilisema taarifa hizi siyo za kweli na jana Serikali ya Tanzania kupitia kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, ilitoa taarifa bungeni na kuziita taarifa hizo kuwa ni za “kupikwa”.
    Wakati hayo yakiendelea, ripoti hiyo ya EIA iliyopewa jina la Vanishing Point: Criminality, Corruption and Devastation of Tanzania’s Elephants (Hatua ya kutoweka: Uhalifu, Rushwa na Kuangamizwa kwa tembo wa Tanzania), inafichua madudu zaidi yanayoweka bayana jinsi uhalifu wa utoroshaji wa meno ya tembo unavyofanyika.
    Ripoti hiyo inalitaja pori la akiba la Selous kuwa kituo cha mauaji ya tembo, kwani matukio ya ujangili hupangwa katika vijiji vinavyozunguka hifadhi hiyo, kisha kutekelezwa kwa msaada wa polisi na baadhi ya wananchi.
    Inavitaja vijiji vilivyopo katika maeneo ya Mloka, Tunduru, Namtumbo, Liwale na Kilwa ambako wafanyabiashara wadogo kutoka Dar es Salaam hukodishwa silaha na wawindaji, kisha kuingia katika hifadhi hiyo na kufanya uhalifu.
    “Wakati mwingine wawindaji kutoka nje ya eneo hilo hutumiwa na baadhi ya maofisa kutoka serikalini,” inasomeka sehemu ya ripoti hiyo.
    Katika tukio la aina yake, ripoti hiyo imeeleza tukio la katikati ya mwaka huu ambapo kundi la wawindaji kutoka Arusha lilitumwa na maofisa wa polisi waliokuwa Mloka na kuingia katika hifadhi hiyo kwa ajili ya kuwinda.
    Inadaiwa kuwa maofisa hao wa polisi walitoa silaha kwa kundi hilo la wawindaji na baada tu ya mauaji ya tembo wapatao watano walichukua meno kutoka kwa wawindaji.
    Kwa mujibu wa ripoti hiyo, tembo akishauawa, meno yake hukatwa kisha kufukiwa hadi pale mnunuzi anapowasili ambapo hufukuliwa na kupewa.
    EIA katika ripoti hiyo inabainisha kuwa meno mengi ya tembo kutoka Selous husafirishwa kwenda Dar es Salaam, ama kwa kutumia barabara kwa maana ya magari ambayo yametengezwa maalumu kwa ajili ya kazi hiyo, au kwa kupitia majini wakitumia mitumbwi ya asili.
    “Wakati mwingine pikipiki hutumika kupitia njia za vichakani kukusanya meno hayo kule ambako zimefichwa hadi kufikia barabara kuu,” inasema sehemu ya ripoti hiyo. Kutoka kwenye njia kuu husafirishwa kwa magari binafsi ambayo yanakuwa sehemu maalumu kwa ajili ya kuficha pembe hizo au kupitia mabasi ambayo husafirisha meno ya tembo zaidi kuliko abiria kutokana na malipo makubwa ambayo hutolewa kwa kazi hiyo.
    Ripoti hiyo inaongeza kuwa: “Kwa kawaida meno ya tembo mabichi yanapofikishwa jijini Dar es Salaam kutoka Kusini huwekwa katika mafungu madogo na kuhifadhiwa katika baadhi ya maeneo kwenye vitongoji vya jiji hilo. Pindi anapotokea mteja anahitaji kununua hukusanywa na kuuziwa”.
    Inaelezwa kuwa kawaida hifadhi hizo huwa katika maeneo ya viwanda kama vile Chang’ombe karibu na bandari, lakini pia wakati mwingine katika viwanja vilivyopo mbali na makazi ya watu.
    Selous hatarini
    Kutokana na hali hiyo, ripoti hiyo inasema Hifadhi ya Selous ipo katika hatari ya kupoteza hadhi yake kutokana na kukithiri kwa matukio ya ujangili, huku Serikali ikionekana kwamba haijali.
    Ripoti hiyo inadai kuwa hifadhi kongwe yenye maeneo makubwa yapatayo kilomita za mraba 50,000 haina ulinzi wa kutosha hali inayotoa mianya kwa makundi ya uhalifu wa wanyamapori kufanya vitendo hivyo.
    EIA inasema idadi ya tembo katika Hifadhi ya Selous imeshuka kutoka 70,406 mwaka 2006 hadi kufikia 13,084 mwaka 2013. Hiyo ikimaanisha kwamba idadi ya tembo 57,322 wameuawa katika kipindi cha miaka saba.
    Mauaji hayo yamethibitishwa kwa kipimo cha vinasaba (DNA) na kubainisha kuwa asilimia kubwa ya mauaji ya tembo yanahusishwa na ukataji wa pembe za ndovu.
    Kwa mujibu wa EIA mwaka 2000 tayari kulikuwa na ishara za wazi zilizoonyesha kuwapo kwa mauaji ya tembo na kwamba baadhi ya vyombo vya habari viliripoti juu ya hali hiyo hasa baada ya mizoga ya tembo kuonekana ikiwa imezagaa katika hifadhi ya Selous. “Lakini, mkurugenzi wa wanyamapori alipoulizwa kuhusiana na hali hilo, alisema kuwa matukio ya ujangili yapo chini,” inasomeka sehemu ya ripoti hiyo yenye kurasa 36.
    Inaendelea kueleza kuwa, mwaka 2010, EIA walitembelea eneo la Selous na kufanya mahojiano na wanakijiji ambao walifichua siri juu ya maeneo yanayotumika kufanyia biashara haramu ya meno ya tembo.
    Njia za magendo zinazotumika kusafirisha meno hayo zinawahusisha polisi na askari wanyamapori ambao taarifa hiyo inawataja kwamba wao ndio waliopaswa kuwa mstari wa mbele kulinda hifadhi hizo, hali inayoifanya EIA kuitupia lawama Serikali ya Tanzania.
    “Licha ya ishara hizi za wazi, Serikali ya Tanzania imeshindwa kupambana na ujangili katika Hifadhi za Selous. Zaidi ya tembo 25,000 waliuawa kati ya mwaka 2010 na mwaka 2013. Sababu kuu iliyosababisha vifo vya tembo hao ni ujangili.
    “Mwaka 2011, theluthi mbili ya mizoga ilionekana katika Hifadhi ya Selous. Sababu inayochangia ni ukosefu wa rasilimali kwa ajili ya kulinda hifadhi kwa umakini,” inasomeka sehemu ripoti hiyo.

    MASHINE ya kurushia matangazo ya BUNGE yaibiwa

    MASHINE ya kurushia matangazo ya moja kwa moja na kuchanganya picha, imeibiwa ndani ya ukumbi wa jengo la Bunge katika mazingira ya kutatanisha, Tanzania Daima limebaini.
    Mashine hiyo (Mixer), mali ya kituo cha Televisheni ya Star TV, imeibiwa ikiwa imehifadhiwa kwenye chumba maalum cha kurushia matangazo ya Televisheni na Radio za vituo mbalimbali baada ya kumalizika kwa Bunge Maalum la Katiba.
    Ingawa thamani halisi ya mashine hiyo haijajulikana, lakini inaelezwa kuwa ina thamani kubwa ya mamilioni ya fedha na haipatikani nchini.
    Mbali ya kuiba mashine hiyo, wajanja hao pia wameiba vingamuzi viwili vilivyokuwa vikitumika wakati wa kurusha matangazo ya moja kwa moja bungeni.
    Uchunguzi uliofanywa na Tanzania Daima, umebaini kuwa mashine hiyo imeibiwa baada ya kumalizika kwa Bunge Maalum la Katiba na hakuna aliyenaswa wala kudaiwa kuhusika na wizi huo.
    Habari za kiintelejinsia kutoka viwanja vya Bunge, zinasema kuwa tayari maofisa usalama wa Bunge wameanza kupitia picha za kamera za Bunge kusaka wezi hao.
    Kutokana na kuibiwa kwa mashine hiyo, matangazo ya Televisheni ya Star TV na zingine zilizokuwa zikishirikiana kutumia kifaa hicho, yameathirika kwani hayako kwenye ubora unaotakikana.
    Wizi huo umeibua maswali kutoka kwa baadhi ya wabunge na watumishi wa Bunge.
    Baadhi ya wabunge walisema kwa namna jengo la Bunge lilivyo, hakuna uwezekano wa mtu kutoka nje ya mazingira ya Bunge kuja kuiba.
    "Milango ya Bunge inaingia kwa kadi maalum na muda wote kamera zinamulika. Mwizi huyo ameingiaje na ametokaje bila kuonekana," alihoji mmoja wa watumishi wa Bunge.
    Katibu wa Bunge, Thomas Kashilila, alikiri kuibiwa mashine hiyo anazo na Bunge imeanza kuzifanyia kazi.
    Alisema anataka kupata maelezo ya kutosha kwa waandishi na wafanyakazi wa Star TV waliokuwa kazini wakati Bunge Maalum la Katiba lilipoahirishwa na namna walivyoamua kuiacha mashine hiyo iendelee kubaki ndani ya jengo la Bunge bila ofisi yake kuwa na taarifa.
    “Kweli kuna hiyo mashine imeibiwa na jana nilipata barua rasmi ya kujulishwa kupotea kwa kifaa hicho. Nimetoa maelekezo kwa askari na wana usalama wa hapa kuanza kufuatilia na hatimaye tutalazimika kuangalia kwenye kamera kuanzia tarehe ya Bunge hilo lilipoahirishwa hadi sasa,” alisema Dk. Kashilila.

    TANZANIA: TAARIFA JUU YA PEMBE ZA NDOVU NA CHINA SIO KWELI


    Tanzania imeshtushwa na ripoti inayoelezea biashara haramu ya meno ya tembo kati ya baadhi ya viongozi wa nchi hiyo na China
    Serikali ya nchi hiyo imesema imesikitishwa na ripoti iliyotolewa na taasisi ya uchunguzi ya mazingira inayodai kwamba majangili wa kichina wakishirikiana na baadhi ya viongozi wa serikali ya Tanzania ndio wanaoangamiza idadi ya tembo kutokana na biashara haramu ya meno ya tembo.
    Inadaiwa kwamba raia wa China walitumia ziara ya rais wao nchini humo kusafirisha kimagendo maelfu ya kilo za pembe za ndovu.
    Kulingana na shirika la utafiti wa mazingira, EIA, Pembe hizo zilinunuliwa wiki moja tu kabla ya ziara ya rais huyo nchini tanzania mwaka jana na zilifichwa katika mifuko ya wanadiplomasia ili zisitambuliwe.
    Msemaji wa serikali Assah Mwambene amemwambia mwandishi wa BBC Aboubakar famau kwamba ripoti kama hiyo zinatatiza jitihada za serikali kukabiliana na uuzaji haramu wa pembe za ndovu.
    credit, bbc