pagead2.googlesyndication.com pagead2.googlesyndication.com

Kujiunga JWTZ

Uandikishaji
Askari
Mtu yeyote ataandikishwa kujiunga na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa sifa zifuatazo: - 

  • Awe raia wa Tanzania
  • Awe na Elimu ya kidato cha nne na kuendelea na awe amefaulu..
  • Awe hajaoa/hajaolewa
  • Awe na umri kuanzia miaka 18 hadi 25
  • Awe na tabia na mwenendo mzuri
  • Awe na akili timamu na afya nzuri
  • Masharti ya Utumishi
  • Askari atapewa nambari ya utumishi baada ya kufaulu mafunzo ya awali.
  • Atalitumikia Jeshi kwa kipindi cha mwanzo cha miaka sita, baada ya hapo atafanya kazi kwa mkataba wa miaka miwili miwili kwa kibali cha Mkuu wa Majeshi.
  • Maafisa
  • Bodi ya Uteuzi wa Maafisa (Officers Selection Board)
    huwafanyia usaili askari wenye elimu ya kidato cha sita na kuendelea toka Vikosini na Shule za askari wapya (Recruitment Schools).
  • Watakaofaulu masailiano hayo hupewa hadhi ya Afisa Mwanafunzi (Officer Cadet), na hupelekwa Chuoni (Tanzania Military Academy) kwa mafunzo ya uafisa kwa muda wa mwaka mmoja.
  • credit:tpdf.mil.tz

    0 comments:

    Post a Comment