London, England. Waziri Mkuu,
David Cameron amebatilisha uamuzi wa Wizara ya Mambo ya Ndani na kuamuru
uongozi wake ufikirie upya wazo la kuruhusu baa kufunguliwa mapema kwa
biashara ya pombe wakati wa mechi ya Kombe la Dunia dhidi ya Italia,
Juni 14 mwaka huu.
Uamuzi wa Cameroon ni baada ya wamiliki wa baa
kunyimwa kibali cha kubadili muda wa kufungua biashara zao katika mchezo
huo unaotarajiwa kuanza saa 5:00 asubuhi.
Watu walio karibu na ofisi ya Cameroon wameeleza
kuwa kiongozi huyo ameamuru pande zote zinazohusika wakiwamo wamiliki wa
baa, polisi na mamlaka za miji wakae pamoja ili kuhakikisha baa
zinafunguliwa wakati wa mchezo huo dhidi ya Italia.
Awali, Wizara ya Mambo ya Ndani ilipinga maombi ya
Chama cha Wauza Bia na Wenye Baa waliotaka muda wa kufungua biashara
zao utazamwe upya wakati wa mchezo huo kwa masilahi ya nchi.
Hata hivyo, katika majibu yake kupitia mtandao wa
kijamii, Twitter, Cameron alisema: “Nimeamuru agizo hilo liangaliwe upya
wakati wa mechi zote za England wakati wa fainali za Kombe la Dunia,
tunahitaji mawasiliano ya pande zote zinazohusika.”
Wamiliki wa Baa waliomba muda wa kufungua
biashara ubadilishwe kutoka Saa 5: 00 hadi 7:00, Juni 14 wakati wa
mchezo huo na kuendelea ili mashabiki kufuatilia mchezo huo. Waziri wa
Mambo ya Ndani, Norman Baker alipinga pendekezo hilo na kuacha jukumu
hilo kwa mmiliki mmoja mmoja kwenye mamlaka za miji ili kutoa leseni kwa
gharama ya Pauni 21 kwa kila mmoja.
MWANANCHI
MWANANCHI
0 comments:
Post a Comment