pagead2.googlesyndication.com pagead2.googlesyndication.com

MIAKA 15 JELA KWA KOSA LA KUBAKA

Na Husna Sheha
MAHAKAMA ya mkoa ya Mfenesini,imemuhukumu mshitakiwa Sharif Makame Haji (19) mkaazi wa Mkokotoni wilaya ya kaskazini 'A', kifungo cha miaka 15 jela baada ya kupatikana na hatia katika makosa mawili ya  kutorosha na kubaka.
Hakimu wa mahakama hiyo, Nassor Ali Salim, alitoa adhabu hiyo baaada ya kuridhishwa na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka.
Kabla ya adhabu hiyo, upande wa mashitaka ulidai hauna kumbukumbu za makosa ya nyuma dhidi ya mshitakiwa, hata hivyo apewe adhabu kali ili iwe fundisho kwa wengine wenye tabia hiyo.
Mshitakiwa kwa upande wake aliiomba mahakama impunguzie adhabu.
Ilidaiwa mnamo tarehe 7 Februari na Februari 12 2012, majira ya saa 2:00 usiku katika maeneo ya Mkokotoni wilaya ya kaskazini 'A' Unguja, bila ya idhini na ridhaa ya wazazi wake alimtorosha msichana wenye umri wa miaka 15 na kumpeleka nyumbani kwa rafiki yake aitwae Pua.
Aidha ilidaiwa baada ya kumtorosha, mshitakiwa alimbaka msichana huyo na kumsababishia maumivu,kitendo ambacho ni kosa kisheria

0 comments:

Post a Comment