Timu
ya wakaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Tume ya Mipango wakitazama bidhaa
zilizokuwa zikitengenezwa na kiwanda cha matairi cha General Tyre. Serikali ina mpango wa kufufua kiwanda hicho ambacho kilisimama
uzalishaji tangu mwaka 2007.
Katibu
Mtendaji wa Tume ya Mipango, Dkt. Philip Mpango (mwenye suti nyeusi) akioneshwa
moja ya mashine zilizokuwa zinatumika kutengenezea matairi katika kiwanda cha General Tyre kilichopo katika jiji la
Arusha na Mwangalizi wa Kiwanda hich, Bw. Leonald Mgoyo. Serikali ina mpango wa
kukifufua kiwanda hicho baada ya kusimama uzalishaji tangu mwaka 2007.
Timu
ya wakaguzi wa miradi wa maendeleo wakiangalia mitambo ya kiwanda cha matairi
cha General Tyre jijini Arusha
Timu
ya wakaguzi wa miradi ya maendeleo na baadhi ya wafanyakazi wa kiwanda hicho
wakifurahia jambo wakati wa ukaguzi huo.
Katibu
Mtendaji wa Tume ya Mipango, Dkt. Philip Mpango (mwenye suti nyusi) akiagana na
Mwangalizi wa Kiwanda hicho, Bw Leonald Mgoyo baada ya ukaguzi wa kiwanda hicho.
Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) Bw.
Gideon Nasari na kushoto kwake ni Naibu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango
anayesimamia Klasta ya Uzalishaji, Bw Maduka Kessy.
Picha na Joyce Mkinga,
Mkuu wa Kitengo cha
Mawasiliano Serikalini,
OFISI YA RAIS, TUME YA
MIPANGO
0 comments:
Post a Comment