pagead2.googlesyndication.com pagead2.googlesyndication.com

TAHADHARI YA MVUA KUBWA


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA UCHUKUZI
MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA


Simu: 255 22 2460735/2460706

FAKSI: 255 22 2460735/2460700 S.L.P. 3056

Barua pepe: met@meteo.go.tz DAR ES SALAAM

Tovuti: www.meteo.go.tz

Unapojibu tafadhali nakili:

Kumb. Na.: TMA/1622 04 Machi, 2014
Taarifa kwa Umma:Vipindi vya mvua kubwa vinatarajiwa. Taarifa Na. 201403-01
Muda wa Kutolewa
Saa za Afrika Mashariki
Saa 10:00 Jioni
Daraja la Taarifa: Tahadhari
Kuanzia:
Tarehe
05 Machi, 2014
Mpaka:
Tarehe
07 Machi, 2014
Aina ya Tukio Linalotarajiwa Vipindi vya mvua kubwa inayozidi milimita 50 ndani ya saa 24 vinatarajiwa.
Kiwango cha uhakika: Wastani (65%)
Maeneo yanayotarajiwa kuathirika
Ukanda wote wa Pwani (Mikoa ya Mtwara, Lindi, Pwani, Dar es Salaam, Tanga pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba).
Maelezo:
Hali hii inatokana na kuimalika kwa mgandamizo mdogo wa hewa mashariki mwa bahari ya Hindi sambamba na kusogea kwa haraka kwa mfumo wa mvua za msimu (ITCZ) hivyo kuongeza kiwango cha unyevunyevu kutoka baharini kuelekea maeneo tajwa hapo juu.
Angalizo:
Wakazi na watumiaji wa Bahari pamoja na mamlaka zinazohusika na maafa, wanashauriwa kuchukua tahadhari stahiki.
Maelezo ya Ziada
Mvua zinazoendelea na zinazotarajiwa kunyesha zinaashiria kuanza mapema kwa mvua za masika katika baadhi ya maeneo ya pwani ya kasikazini ikiwemo Dar es Salaam.
Mamlaka ya Hali ya Hewa inaendelea kufuatilia hali hii na itatoa mrejeo kila itakapobidi.

0 comments:

Post a Comment