pagead2.googlesyndication.com pagead2.googlesyndication.com

Hivi ndivyo Chege, Mh. Temba walivyo funika Coco Beach

Chege, Mh. Temba wafunika Coco Beach KATIKA kusherehekea Sikukuu ya Pasaka, wasanii Chege Chigunda ‘Mtoto wa Mama Saidi’ na Mhe. Temba, wametoa burudani ya aina yake kwa wapenzi na mashabiki wa muziki katika tamasha maalumu la ‘Cheka Bombastik’ lililofanyika katika fukwe za Coco, jijini Dar es Salaam.
Burudani hiyo ya nguvu, ilianza kwa staili ya aina yake kwa wasanii chipukizi maarufu kupanda jukwaani na kumwaga burudani ya nguvu kwa maelfu ya mashabiki waliojitokeza.
Kwa ujumla, uwanja ulikuwa umefurika hasa ulipofika muda wa Chege kupanda jukwaani na kuwapeleka mashabiki wake ‘Uswazi Take Away’, akifanya kazi yake vema na kutoa burudani ya kipekee akifuatiwa na Mhe Temba ambaye kwa pamoja waliimba nyimbo kadhaa za Wanaume Halisi.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumalizika kwa tamasha hilo, Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania, ambao ndio waandaaji wa tamasha hilo, Matina Nkurlu, alisema imekuwa kawaida kwa kampuni yao kutoa burudani kwa wakazi wa Dar es Salaam na sehemu nyingine katika ziku za sikukuu.
“Umekuwa ni utaratibu wetu kutoa burudani kwa Watanzania ambao wamekuwa wakituunga mkono na kutufanya kuwa namba moja kila siku,” alisema Nkurlu.
Meneja huyo alisema burudani hiyo ni ya siku mbili (Aprili 20 na 21), na wateja wa Vodacom watakaojitokeza watapata zawadi mbalimbali na wataunganishwa na huduma ya Cheka Bombastik bure ili kupiga simu kwa bei nafuu.

0 comments:

Post a Comment