pagead2.googlesyndication.com pagead2.googlesyndication.com

Hivi ndivyo walivyokamatwa na heroin kwenye kondomu.

VIJANA wawili wenye asili ya kiasia, wakazi wa jiji la Arusha, wametiwa mbaroni na polisi mkoani hapa kwa tuhuma ya kukutwa na kete 170 za dawa za kulevya aina ya heroin na bangi kete 300.
 
Walihifadhi dawa hizo kwenye mfuko mweusi aina ya sandarusi na zingine kete 170 zikiwekwa kwenye mpira wa kiume (kondomu) ndani ya gari.
 
Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Liberatus Sabas aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Mavan Tapel (20) na Nisha Patel (26), wote wakazi wa nyumba za Shirika la Nyumba (NHC) eneo la Metropole jijini Arusha.
 
Sabas alidai vijana hao walikutwa na misokoto 300 ya bangi, kete 170 za heroin zilizokuwa kwenye mfuko wa sandarusi na kete 150, zilizowekwa kwenye kondomu ya kiume.
 
polisi 1
Alisema watuhumiwa hao, walikuwa wakitumia gari aina ya Nissan Primera, ambalo lilitumika kuhifadhi dawa hizo za kulevya.
 
Watuhumiwa bado wanaendelea kuhojiwa katika kituo cha polisi jijini hapa, kutokana na upelelezi wa tukio hilo kutokamilika. Hata hivyo, alisema thamani ya dawa hizo, hazikuweza kufahamika mara moja.

>>Habari leo

0 comments:

Post a Comment