Milipuko miwili imetokea katika
kituo cha mabasi katika vitongoji vya mji mkuu wa Nigeria, Abuja, na
kuna taarifa ya watu wengi kujeruhiwa kwa mujibu wa watu walioshuhudia
tukio hilo.
Mwandishi wa BBC, nchini Nigeria, Haruna Tangaza
anasema milipuko hiyo ilitokea wakati abiria wakiwa katika harakati za
kupanda mabasi na teksi wakienda maofisini katikati ya mji wa Abuja.Mmoja wa mashuhuda wa shambulio hilo, Badamsi Nyanya ameiambia BBC kuwa ameona miili 40 ikiondolewa.
"Asubuhi hii kulikuwa na mlipuko katika eneo la maegesho ya magari ya Nyanya Motor Park," anasema Manzo Ezekiel wa Wakala wa Usimamizi wa Taifa wa Majanga.
Vikosi vya uokoaji tayari vipo katika eneo la tukio.
Shuhuda mwingine Bi Mimi Daniels, ambaye anafanya kazi mjini Abuja, anasema: "nilikuwa nasubiri basi niliposikia mlipuko mkubwa halafu nikaona moshi," ameiambia Reuters.
"Watu walikuwa wakikimbia ovyo kutokana na taharuki."
BBC
0 comments:
Post a Comment