pagead2.googlesyndication.com pagead2.googlesyndication.com

Mafuriko yawavagaa Wafungwa Keko

MVUA zinazoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam zimewaweka mahabusu na wafungwa katika Gereza la Keko katika hali ngumu kutokana na gereza hilo kuvuja.
Habari kutoka kwa askari magereza wa gereza hilo, zinaeleza wafungwa wamekuwa wakipata tabu kutokana na kukosa mahali pa kulala na muda wote wakiwa wanakausha maji yanayoingia ndani ya gereza hilo.
Askari hao waliliambia Tanzania Daima kuwa jengo namba 3, 4, 5 na selo namba  4, 5, 6, 7, 8, 9 na 10 zote zinavuja na kuwafanya mahabusu na wafungwa kushindwa kulala.
“Hapa karibu block zote zinavuja, ni za zamani toka enzi za mkoloni na kuwafanya mahabusu na wafungwa kushindwa kulala,” alisema askari mmoja ambaye hakutaka kutajwa jina gazetini.
Alisema karibu kila jengo linavuja hata katika jengo la utawala ambalo waliamua kuezeka mabati.
Akizungumza na Tanzania Daima kwa njia ya simu kuhusu suala hilo, Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Magereza (ACP), George Mwambasha,    alisema hawajapata taarifa zozote zile labda afike katika eneo hilo aangalie hali ikoje.
“Sisi hatujapata taarifa zozote zile labda hadi niende Keko niangalie ndiyo naweza kusema lolote kuhusiana na hilo,” alisema Mwambasha.
freeemedia

0 comments:

Post a Comment