pagead2.googlesyndication.com pagead2.googlesyndication.com

Wakimbizi wauawa katika kambi ya UN


Wakimbizi wauawa katika kambi ya Umoja wa Mataifa Sudan Kusini
Afisa mkuu wa Umoja wa mataifa nchini Sudan kusini Tobby lanzer ameiambia BBC kuwa makumi ya wakimbizi wa ndani ya nchi hiyo iliyosakamawa na vita vya wenyewe kwa wenyewe wameuawa ndani ya kambi ya Umoja wa
mataifa iliyoko katika mji mkuu wa jimbo la Jonglei BOR .
Afisa anayesimamia shughuli za utoaji misaada ya umoja wa mataifa nchini sudan toby Lanzer amesema kuwa kundi la vijana wanaokisiwa kuwa zaidi ya mia tatu hivi walikuja katika kambi hiyo wakidai kuwa walitaka kuwasilisha
malalamiko, kwa wasimamizi wa kambi hiyo. Toby alisema '' Ilikuwa mwendo wa saa nne hivi katikati ya mji mkuu wa jimbo la jonglei BOR ambapo vijana takriban 350 hivi walikusanyika na kuanza kuandamana hadi kwenye ua la
kambi yetu mara wakavunja lango kuu na kuingia ndani ya kambi .
Maafisa wetu walifyatua risasi ilikuwatawanya lakini wao pia wakaanza kufyatua risasi kiholela na katika tafrani iliyotokea wavamizi hao waliwashambulia wakimbizi waliokuwa wametorokea katika kambi yetu wakati wa
mapigano yaliyozuka desemba .'
Wakimbizi wauawa katika kambi ya Umoja wa Mataifa mjini Bor
W,mjini BorAfisa huyo alilaani tukio hilo akisema ni jambo la kuhuzuzisha kwa watu waliokimbilia usalama ndani ya kambi ya umoja wa mataifa wakivamiwa humohumo na kuwa Umoja wa mataifa sasa utachukua
tahadhari zaidi ilikuzuia matukio kama hayo katika siku za usoni.
''Tumeimarisha hali ya usalama katika kambi zetu ilikuwazuia wale wote wenye niya ya kutudhuru sisi na kuanzia sasa tunatoa tahadhari kwa makundi yote kuwa tutatumia nguvu kadri na uwezo wetu ilikuzuia matukio kama haya
na kulinda maisha ya wale wote ambao wametorokea hapa ilikuokoa maisha yao''.
Maafisa 2 wa kulinda usalama wa umoja wa mataifa walijeruhiwa vibaya katika shambulizi hilo.
Kambi ya BOR imehifadhi zaidi ya wakimbizi 5000 tangu mwezi Desemba majeshi ya serikali ya rais Salva Kiir yalipoanza makabiliano na makundi ya wapiganaji wanaomuunga mkono aliyekuwa makamu wa rais wa nchi hiyo Riek
Machar.

0 comments:

Post a Comment