Mashirika ya usalama ya Israel yametoa ripoti na kueleza kuwa
sababu kuu iliyolilifanya jeshi la utawala huo kushindwa katika vita
ilivyoanzisha huko Ghaza ni taarifa zisizo sahihi na kushindwa
kukabiliana na muqawama wa Palestina. mashirika ya usalama ya utawala wa
Kizayuni likiwemo shirika la taarifa za ndani la Israel(Shabak) na
shirika la taarifa za kijeshi (Aman) yamechapisha ripoti na kufichua
kuwa, jeshi la Israel liligonga mwamba katika kupata taarifa yoyote
kuhusu mahali walipo makamanda wa muqawama wa Palestina na hata viongozi
wa kisiasa wa Palestina huko Ghaza.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo,mashambulizi ya Israel huko Ghaza
hayakuzaa matunda kwa mujibu wa viwango vyote vya kijeshi au
kiitelijinsia na kwamba vita hivyo vimeonyesha kuwa utawala wa Kizayuni
hauna taarifa za kweli kuhusu matukio ya Ghaza.
0 comments:
Post a Comment