Stori: Haruni SanchAwa
NIkweli imetokea! Ni kwenye Kanisa la Paradise Internation Ministries lililoko Karakata Ukonga jijini Dar, mwanamke mmoja (pichani) anayedaiwa mchawi alidondoka usiku wa saa saba na kujikuta hawezi kutembea.

Tukio hilo lilijiri Septemba 13, mwaka huu wakati waumini wa kanisa hilo wakiwa wamezama kwenye maombi ya kufunga.
Ilidaiwa kuwa, waumini wa kanisa hilo wakiwa katika maombi hayo, Nabii Gideon Parapanda aliwahakikishia kuwa…
Stori: Haruni SanchAwa
NIkweli imetokea! Ni kwenye Kanisa la Paradise Internation Ministries lililoko Karakata Ukonga jijini Dar, mwanamke mmoja (pichani) anayedaiwa mchawi alidondoka usiku wa saa saba na kujikuta hawezi kutembea.
NIkweli imetokea! Ni kwenye Kanisa la Paradise Internation Ministries lililoko Karakata Ukonga jijini Dar, mwanamke mmoja (pichani) anayedaiwa mchawi alidondoka usiku wa saa saba na kujikuta hawezi kutembea.
Tukio hilo lilijiri Septemba 13, mwaka huu wakati waumini wa kanisa hilo wakiwa wamezama kwenye maombi ya kufunga.
Ilidaiwa kuwa, waumini wa kanisa hilo wakiwa katika maombi hayo,
Nabii Gideon Parapanda aliwahakikishia kuwa usiku huo kutatokea mambo ya
ajabu kufuatia maombi hayo.
Inadaiwa ilipofika saa saba usiku mwanamke huyo akiwa na wenzake
watatu, walidondokea kanisani hapo na kusababisha taharuki kwa waumini
waliokuwa wakifanya maombi ndani. Mwanamke huyo alikuwa na kitambaa
chekundu kikidaiwa ni hirizi, fimbo nyeusi iliyozungushiwa shanga na
alikuwa amejipaka masizi mwilini.
Mwanamke baada ya kudondokea kanisani na kusababisha taharuki kwa waumini waliokuwa wakifanya maombi ndani.
Akizungumza na Uwazi, Nabii Parapanda alisema watu hao walidondoka
watatu, wawili walifanikiwa kukimbia akabaki huyo mmoja
aliyejitambulishwa kwa jina moja la Aisha, mkazi wa Mwananyamala A
jijini Dar.
Baada ya tukio hilo vyombo vya ulinzi, askari wa JWTZ na polisi
walifika kwa lengo la kuhakikisha usalama wa eneo hilo lakini nabii
huyo aliomba mtu huyo asichukuliwe hadi atapofanyiwa maombi maalum.
Ombi la kiongozi huyo lilikubaliwa ambapo Aisha alipandishwa
madhabahuni na kukiri kuwa alikuwa na wenzake watano lakini katika
kuanguka walikuwa watatu, wawili walifanikiwa kukimbia bila kusema
walikuwa wakitoka wapi kwenda wapi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Ilala, SACP Mary Nzuki alipohojiwa kuhusiana na tukio hilo alisema:
“Ni kweli tukio hilo limetokea na watu wameshuhudia, mwanamke huyo bado yuko kanisani hapo kwa maombi.”

0 comments:
Post a Comment