Matukio
ya mauaji ya watu wasio na hatia, yameendelea kuuandama Mkoa wa Geita,
kufuatia watu watatu kuuawa kwa kukatwa mapanga na kuchomwa mkuki huku
mmoja akijeruhiwa baada ya mtu mmoja anayesadikiwa ni mgonjwa wa akili
kutekeleza unyama wake.
Tukio
hilo lililotokea jana asubuhi katika kijiji cha Nyamilyango wilayani
Geita, na aliyejeruhiwa na kulazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Geita
ni Mathayo Sindamsanga, na hali yake imeelezwa ni mbaya. Mganga Mfawidhi
wa hospitali hiyo, Dk. Adam Sijaona, alithitibisha kupokea miili mitatu
iliyohifadhiwa hospitalini hapo pamoja na majeruhi mmoja.
Dk. Sijaona aliwataja waliouawa kuwa ni Pindo Makono, Ndakazi Bertha Masabile na Jacob Bukulu, ambao ni wakazi wa kijiji hicho.
Hata hivyo, mtu huyo aliyesababisha mauaji hayo, alikamatwa na wananchi wenye hasira na kisha kumfikisha kituo cha polisi.
Dk.
Sijaona alisema marehemu hao walifariki dunia kutokana na kuvuja damu
nyingi mwilini kufuatia muuaji kutumia panga na kuwacharanga na kisha
mkuki kuwatoboa miili.
Akizungumzia
tukio hilo, Diwani wa Kata ya Bugulula, Elisha Lupuga, alisema
lililotokea juzi saa 1:00 jioni katika kitongoji cha Misheni katika
kijiji cha Nyamilyango baada ya mtuhumiwa, Rashid Ramadhani, mkazi wa
kijiji hicho kutumia mkuki na panga kuwaua watu hao.
“Dhamira
yake mpaka sasa haijafahamika ilikuwa nini, lakini amekuwa na tabia ya
kuvuta bangi kwa muda mrefu, hivyo tunahisi amevurugukiwa akili yake,” alisema Lupuga.
Hata
hivyo, Lupuga alisema baadhi ya waliouawa walikuwa na mahusiano na
mtuhumiwa, lakini hakufafanua ni mahusiano ya namna gani waliyokuwa
nayo.
Kamanda
wa Polisi wa Mkoa wa Geita, Joseph Konyo, alithibitisha kutokea tukio
hilo na kwamba mtuhumiwa anashikiliwa katika kituo cha polisi akisubiri
hatua za kisheria kuchukuliwa dhidi yake.
Tukio
hilo limeibua upya simanzi na vilio kwa wananchi wa mkoa huo ambao mara
kwa mara wamekuwa wakikumbwa na matukio ya mauaji ya aina mbalimbali.
Hilo
ni tukio la pili ndani ya wiki moja baada ya usiku wa kuamkia Septemba
7, mwaka huu, watoto wanne wa familia moja kuuawa kufuatia nyumba yao
kuteketezwa na moto katika kitongoji cha Elimu kata ya Kiangalala
wilayani Geita.
Watoto
walioteketea na moto huo ni Reginald Robert (9) mwanafunzi wa darasa la
nne na Sofia (6) wa Shule ya Msingi Ukombozi na Remijius (4) wa
chekechea pamoja na Scolastika (15) aliyekuwa akisoma shule ya sekondari
Mwatulole.
Katika
tukio hilo, baba wa familia, Robert Reginald (49), mkewe Angelina
Reginald na watoto Robert mwenye umri wa miaka miwili na miezi mitatu na
Yohana (1), walinusurika katika janga hilo.
0 comments:
Post a Comment