mfano wa wanafunzi madrasa
Madina
Issa na Khamisuu Abdallah
Wakati Serikali na taasisi za kiraia zikiendelea kukemea vitendo vya udhalilishaji,
bado viunaendelea kushamiri.
Katika
tukio la hivi karibuni mwanafunzi mwenye umri wa miaka 11 (jina linahifadhiwa)
anadaiwa kudhalilishwa na mwalimu wake wa madrasa.
Mtuhumiwa
wa tukio ametajwa kwa jina la Seif Nassor anaefundisha chuo cha Almadrasatu
Ayatul- Atfar, kilichopo Mpendae.
Mwalimu
huyo anaaiwa kumuingilia mtoto huyo kinyume cha maumbile.
Akizungumza
na ZanzibarLeo katika kitengo cha mkono kwa mkono hospitali kuu ya Mnazimmoja
ambako alifikishwa kupatiwa matibabu, mtoto huyo alisema mwalimu wake amekuwa
na tabia ya kumchukua ofisini na kumwambia avue nguo zote na alale chini na
baadae kumpitishia uume wake.
“Mwalimu
Seif huwa ananiita ofisini kabla wanafunzi hawajatolewa na kukomea mlango kwa
juu kisha ananambia nivue nguo zote na nilale chini kisha ananiingiza uume wake
nyuma kisha ananambia nivae nguo,” alisema.
Alisema
mbali na yeye pia kuna watoto wengine wamekuwa wakifanyiwa vitendo hivyo na
mwalimu huyo.
Alisema siku ya mwisho kufanyiwa kitendo hicho
ilikuwa Jumapili kabla ya mwalimu huyo kuondoka.
Mama
mzazi wa mtoto huyo (jina linahifadhiwa) alisema taarifa ya mtoto wake
kudhalilishwa, alizipata kutoka kwa jirani yake ambae watoto wake wanasoma chuo
hicho.
Alisema
alipokwenda kumuuliza mtoto wake alikiri kufanyiwa vitendo hivyo.
Alisema
mwalimu huyo amekuwa na tabia ya kwenda nyumbani kwa mtoto huyo kila
kunapokucha ambapo siku ya Septemba 7 alikwenda kuwaaga na kuelekea kisiwani
Pemba.
Hata
hivyo, alisema anashindwa kutoa taarifa kwa uongozi wa chuo kwa sababu
wanamuwekea kifua mwalimu huyo.
Aliiomba
serikali kutoa adhabu kali kwa wafanyaji wa vitendo hivyo kwani vinaongezeka
siku hadi siku.
Daktari
wa kitengo hicho ambae alimfanyia uchunguzi mtoto huyo, Salum Omar Mbarouk,
alisema alimpokea mtoto huyo na kumchunguza na kugundua kwamba sehemu zake za
siri zipo salama.
Alitoa
wito kwa wazazi na walezi kuwa waangalifu na watoto wao wanapotoka majumbani
kwani vitendo vya ubakaji vimezidi.
0 comments:
Post a Comment