
Tukio hilo ni la jana saa 5 asubuhi, ambapo wakati Ahmadi
anajinyonga, familia yake ilikuwa nyumba ya jirani kwenye shughuli ya
Maulid.
Mama mkubwa wa Ahmadi, Sikujua Saidi, alisema jana asubuhi walikwenda na Ahmadi kuchuma korosho maeneo ya barabarani.
Baada ya kumaliza, alimuaga kuwa anarudi nyumbani na alimruhusu.
Baada ya kurudi nyumbani, alikuta mlango uko wazi na alipoingia ndani,
alimuona Ahmadi ananing’inia.
Alimuita lakini hakuitikia na ndipo akatoka nje kwenda kuwaita
majirani kwenye Maulid ili waje wamwangalie na walipofika walibaini
ameshapoteza maisha.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Augustine Olomi, alipotafutwa kwa njia ya simu kuthibitisha, alikiri kutokea kwa tukio hilo.
Alisema maofisa wake, wameshakwenda eneo la tukio na atatoa taarifa kwa vyombo vya habari baadaye.
0 comments:
Post a Comment