pagead2.googlesyndication.com pagead2.googlesyndication.com

West Brom na Man U hapatoshi leo

Leo tunashuhudia mtanange mwingine mkali kati ya West Brom na Manchester United itakayomkosa Wayne Rooney anayetumikia adhabu ya Kadi nyekundu.
Yako mambo ya kukumbukwa zinapokutana timu hizi mbili, West Brom iliwahi kuwachapa United mara moja tu katika Premier League.
Leo ni jumatatu ni vema kukumbuka kuwa West Brom imeshinda mechi mbili tu kati ya 18 ilizocheza katika siku ya jumatatu na wakipata bao moja watatimiza magoli 500 katika Premier League.
West Brom wakiwa kwao wamepoteza mchezo mmoja tu katika mitano ambapo walishinda michezo miwili na kutoka sare michezo miwili.
Upande wa Manchester United wakishinda mechi ya leo utakuwa ni ushindi wao wa tatu mfululizo katika mwaka huu.
Lakini wakiupoteza mchezo wa leo itakuwa ni mechi ya tano kuipoteza katika mchezo wao wa nje ambayo ni matokeo mabaya ndani ya miaka mitano. Ni miaka 18 iliyopita tangu Manchester United ilipopoteza michezo sita bila ushindi katika Premier League.

0 comments:

Post a Comment