SHIRIKA la ndege kutoka Falme za Kiarabu (Etihad Airways), limezindua safari za kila siku kutoka Abu Dhabi hadi Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari kwenye hafla ya uzinduzi wa ofisi
za Etihad Airways mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam, Makamu wa Rais
wa Shirika hilo, Moris Pholeli, alisema safari hizo zitaanza rasmi
Desemba mosi mwaka huu.
“Dar es Salaam ni moja ya miji inayokua kwa kasi duniani na sisi
tumeamua kuingia katika soko, kwa kuanzia tutatumia ndege aina ya Airbus
A320 na 16 Business Class na 120 yenye daraja la uchumi,” alisema.
Alisema kuwa, Dar es Salaam itakuwa ni kituo cha 110 kwa ndege za
Etihad duniani na kituo cha 11 katika Afrika na Bahari ya Hindi.
Alibainisha kuwa, Falme za Kiarabu na Tanzania kati ya mwaka 2007 na
2012, zimefanya biashara ya kuridhisha ambako imeongezeka maradufu na
kufikia dola milioni 761 za Marekani.
0 comments:
Post a Comment