Katika taarifa ya kituo cha ITV,
kuna taarifa ya kuhusu kuwasili kwa mabehewa mapya 50 ya treni,
akizungumza wakati wa kuwasili mabehewa hayo Katibu Mkuu Wizara ya
Uchukuzi amesema; “…Rai yangu kubwa kwa
Watanzania na wafanyakazi TRL, mali hizi zinazoletwa ni za kwetu tuwe
watu wa pamoja kulinda mali hizi kwa namna moja au namna nyingine. Kila
Mtanzania Reli inakopita awe ni mmoja wa kushiriki katika ulinzi wa Reli
hii kwa sababu tunaamini kabisa usafirishaji wa mizigo kwa njia ya Reli
ambao umeanza sasa hivi unatupeleka katika matokeo makubwa ambao faida
yake itapatikana kwa Tanzania wakulima kwa kusafirisha mizigo…”– Shaban Mwinjaka
Naye Mkurugenzi Mkuu wa TRL amesema; “…
Leo kuna hizi behewa 50 baada ya muda mfupi katika mwezi huu unaokuja
wa Desemba kutakuwa na behewa 50 zingine kati ya hizo 274, mwezi huo huo
Desemba kuna 50 zingine, mapema mwakani kuna behewa 174… baadaye
kutakuwa na Locomotive mpya na kadhalika. Kuna miradi kama 12 ambayo
TRL inatekeleza sasa hivi katika program ya BRN, hizi behewa 274 ni
sehemu tu lakini kuna Locomotive mpya, mabehewa ya abiria mapya ambayo
nayo mwanzoni mwa Desemba yatafika tutakutana, tutayaona…”–Mhandisi Kipalo Kisamfu
0 comments:
Post a Comment