
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amemtumia salamu za
pongezi Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa mnasaba
wa maadhimisho ya miaka 36 ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu. Katika
ujumbe wake huo, Rais Jakaya Kikwete amempongeza Rais Rouhani na taifa
la Iran kwa ujumla kwa mnasaba wa maadhimisho ya miaka 36 ya ushindi wa
Mapinduzi ya Kiislamu yaliyofikia kilele hapo jana. Ujumbe huo
uliotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ya
Tanzania umemnukuu Rais Kikwete akiitakia kila la kheri Jamhuri ya
Kiislamu ya Iran katika maadhimisho ya mwaka wa 36 ya ushindi wa
Mapinduzi ya Kiislamu yaliyotokea mwaka 1979 kwa uongozi wa Imam
Ruhullah Khomeini (M.A).
Rais Kikwete amesisitiza katika salamu zake hizo za pongezi kwamba,
Tanzania na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran zina uhusiano mkongwe, wa
kihistoria na wa kiutamaduni. Amesema Dar es Salaam na Tehran zina
ushirikiano mzuri katika nyuga mbalimbali na kwamba, ana matumaini nchi
mbili hizi zitapanua zaidi ushirikiano wao katika sekta nyingine kama za
usafiri, biashara, uwekezaji, teknolojia, mafuta, gesi na mawasiliano.
Ikumbukwe kuwa, jana ilikuwa kilele cha maadhimisho ya ushindi wa
Mapinduzi ya Kiislamu hapa Iran, ambapo mamilioni ya wananchi
waliandamana na kutangaza tena himaya na uungaji mkono wao kwa Mapinduzi
ya Kiislamu na mfumo wa Kiislamu unaotawala hapa nchini.
0 comments:
Post a Comment