Hatimaye mbunge wa Monduli nchini
Tanzania, Edward Lowassa, amesema ameshawishika kugombea urais wa nchi
hiyo kwa tiketi ya chama cha CCM na ametangaza rasmi kuwa, atachukua
fomu ya kugombea urais kwa tiketi ya chama hicho tawala. Lowassa ambaye
alikuwa Waziri Mkuu wa Serikali ya Awamu ya Nne huko Tanzania, kwa muda
mrefu amekuwa akitajwa kuwa mmoja wa makada wa CCM wenye nia ya kugomea
urais, lakini hakuwahi kutangaza nia ya kuwania nafasi hiyo. Lakini
jana, alizungumzia suala la urais ambalo lilimfanya yeye na wenzake
watano wafungiwe kwa kipindi cha miezi 12 kujihusisha na harakati hizo
baada ya Kamati Kuu ya CCM kuwatia hatiani kuwa walianza kampeni mapema
kabla ya muda kufika. "Nimepata barua za ushawishi kutoka kwa watu
wengi, lakini nyinyi nimeshawishika," alisema Lowassa nyumbani kwake
mjini Dodoma wakati alipokuwa anazungumza na masheikh wa misikiti ya
Wilaya ya Bagamoyo wanaokadiriwa kufikia 50 ambao pia walikwenda mjini
humo kwa ajili ya kumshawishi aingie kwenye kinyang'anyiro cha urais na
kumkabidhi mchango wa Sh700,000 kwa ajili ya kuchukulia fomu.
0 comments:
Post a Comment