pagead2.googlesyndication.com pagead2.googlesyndication.com

Muvi Ya Kessy kesho Episode Ya Mwisho


SIKU chache baada ya Kamati ya Sheria na Hadhi ya Wachezaji kumwidhinisha Hassan Kessy kuichezea Yanga, sarakasi za beki huyo bado zinaendelea na sasa hatma yake itajulikana kesho.
Agosti 23 ikiwa ni siku chache baada ya Kamati ya Sheria na Hadhi ya Wachezaji chini ya Richard Sinamtwa kumuidhinisha Kessy kucheza Yanga, Simba iliwasilisha malalamiko yao ikitaka Kessy awalipe fidia ya dola 600,000 sawa na Sh bilioni 1.2.
Pia mapema wiki iliyopita, kamati hiyo ilikutana ikiwa na viongozi wa Simba, Chama cha Wachezaji wa zamani (Sputanza) hata hivyo kikao hicho hakikufikia muafaka.
“Simba wamefungua kesi mbili, kesi moja dhidi ya Yanga kumrubuni Kessy na kusaini kwenye timu yao kinyume na taratibu wakati kesi ya pili wamemfungulia Kessy mwenyewe,”alisema Msemaji wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Alfred Lucas.
Katika mashtaka hayo ya Simba ni pamoja na kufanya mazoezi na Yanga, kusajili kwenye klabu hiyo ya Jangwani akiwa ndani ya mkataba na pia kusafiri na Yanga kwenda Uturuki kambini wakati timu hiyo inajiandaa na mchezo wao wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Algeria.
Lucas alisema tayari TFF wameiandikia barua Yanga ambayo ilikacha kikao cha kwanza na kwamba iwapo Jumapili isipotokea basi kesi hiyo itasikilizwa upande mmoja na kutolewa uamuzi.
Kessy alisajiliwa na Simba misimu miwili iliyopita kutoka Mtibwa Sugar ya Morogoro kwa mkataba wa miaka miwili akilipwa Sh milioni 20, hata hivyo ligi ya msimu uliopita ikiwa inaelekea ukingoni, beki huyo alitofautina na viongozi wake ambao walimpa adhabu ya kukaa benchi hadi ligi itakapomalizika.
Kessy hakuafikiana na hatua hiyo na kuamua kujiunga kwa wapinzani wao, Yanga, na kwa mara ya kwanza aliichezea timu hiyo ya Jangwani katika mchezo wa Ngao ya Hisani kati ya Yanga na Azam Agosti 17 na kuikosesha timu hiyo penalti.

0 comments:

Post a Comment