Abiria
hao walikuwa wanasafiri na gari dogo aina ya Toyota Pick Up namba T 170
AKZ kwenda kuhani msiba uliotokea katika kijiji cha Kongei kilichoko
Hedaru mkoani Kilimanjaro.
Kwa
mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kilimanjaro , Robert Boaz
waliofariki ni Stella John (45), Salma Kizoka (33), Marry Senzige (49),
Neema Daniel (52), Rehema George, (29), Sophia Mbike (51), Ritta Kallani
(55) na Kallan Stephano (55), Kolina Mmasa (55) na Bahati Daudi (25),
Wengine
ni Farida Kiondo (24) na Maria John (33) wote wakazi wa Kongei na
kwamba miili yao imehifadhiwa katika hospitali ya Wilaya ya Same.
Boaz
aliwataja majeruhi kuwa ni Zubeda Mrindoko (42),Mipa Chediel (29) na
Zubeda Mlita (32) ambao wamelazwa katika hospitali ya rufaa ya KCMC
kutokana na hali zao kuwa mbaya zaidi.
Wengine waliolazwa hospitalini Same ni Joyce Kandogwe (29), Subira Juma (22), Ramadhan Msangi (31) na Adinan Rajab (31).
Ajali
hiyo ilitokea juzi saa 2:00 usiku katika barabara kuu ya Tanga-Moshi,
nje kidogo ya mji wa Hedaru, ikihusisha magari matatu ambayo ni Fuso (T
299 ANM) ikitokea Moshi kwenda Dar es Salaam na Scania (T 737 AKW)
pamoja na tela lake namba T 776 CCN ikitokea Dar es Salaam kwenda Moshi,
kwa mujibu wa Mkuu wa Wilaya ya Same, Herman Kapufi.
Alisema
watu hao walikuwa wamepanda gari la Diwani wa Kata ya Hedaru (CCM),
Gerald Gwena aliyekuwa amewapakia waombolezaji hao kwenye pick-up yake
ambayo iligongwa kwa nyuma na Fuso na baadaye gari hilo kuparamiwa kwa
nyuma na Scania na kisha kusababisha vifo na majeruhi.
"Waombolezaji
hawa walikuwa wanakwenda na diwani kuifariji familia ya marehemu mzee
Mwanga ambaye mtoto wake wa kiume, Dismas Mwanga alifariki baada ya
kusombwa na mafuriko”, alisema.
Alisema
Dismas mwenye miaka tisa aliyekuwa anachunga kondoo milimani alifariki
dunia juzi mchana baada ya kusombwa na mafuriko yaliyotokana na mvua
kubwa zilizonyesha mfululizo.
Alisema hata, hivyo mpaka sasa haijafahamika iwapo mvua hizo zimesababisha vifo na hasara nyingine.
Kapufi alisema kamati yake ya ulinzi na usalama imekutana kwa dharura kujadili ajali hiyo na hatua ambazo wilaya hiyo itachukua.
Kamanda
Boaz, alisema chanzo cha ajali hiyo ni kuzimika ghafla kwa gari hilo
mali ya diwani Gwena ambaye alikimbia baada ya ajali hiyo.
"Ajali
hiyo ilitokea baada ya gari hilo kuzimika na Fuso iliyokuwa karibu
kuteleza barabarani baada ya kujaribu kusimama ili isigongane na Pick Up
iliyokuwa na waombolezaji, lakini lilivutwa na tope lililokuwa limejaa
barabarani kisha kugonga kabla ya kupinduka na kuangukia upande wa kulia
wa barabara ambako kulikuwa na lori la Scania.
Kamanda alisema watu 10 walikufa papo hapo , wawili walifia hospitalini na saba wamejeruhiwa.
Alisema juhudi za kuwasaka madereva hao wa Fuso pamoja na diwani huyo zinaendelea.
0 comments:
Post a Comment