Maandamano ya kupinga ubakaji India
Wanaume watatu wamehukumiwa kifo
Mjini Mumbai, India baada ya kupatikana na hatia katika visa tofauti
vya ubakaji walioufanya kwa pamoja.
Moja ya visa hivyo kilitokea dhidi ya mwandishi mpiga picha aliyekuwa kazini alipobakwa.Sheria hiyo ilipitishwa baada ya kile kisa Delhi kilichoughadhabisha umma cha msichana aliyebakwa na ngege basini na kujeruhiwa vibaya sana.
Wanaume hao walikuwa wameshitakiwa kwa kesi ya kumbaka msichana huyo mwandishi aliyekuwa ameenda kupiga picha kiwanda cha nguo kilichotelekezwa, lakini pia mwanamke mwengine akajitokeza na kutoa ushahidi wa jinsi wanaume hao walivyombaka maeneo hayo hayo mwezi mmoja kabla.
Wahukumiwa hao wanaweza kukata rufaa kwa mahakama ya juu zaidi.
Kuongezaka kwa visa vya ubakaji vimepelekea maaandamano ya mara kwa mara nchini humo na sasa mahakama zinaharakisha kusikilizwa kwa kesi hizo.
Pia limekuwa swala la mijadala mikali katika kampeni za uchaguzi unatajariwa hivi karibuni nchini humo.
bbc
0 comments:
Post a Comment