KLABU ya Villarreal imempiga marufuku ya kudumu ya kutoingia
katika uwanja wake wa El Madrigal shabiki aliyemrushia ndizi beki wa
kulia wa FC Barcelona, Dani Alves kwenye mchezo wa La Liga jana
jumapili.
Beki huyo wa kibrazil baada ya kurushiwa ndizi hiyo aliiokota na
kuila wakati akiwa katika harakati za kupiga kona, na kitendo hicho
kilionesha shukurani za kejeli kwa shabiki aliyefanya jambo hilo la
kibaguzi.
Katika mechi hiyo Barca walitoka nyuma kwa mabao 2-0 na kushinda 3-2.
Villarreal wamethibitisha kumpa kifungo cha kidumu shabiki huyo na
kusitisha tiketi zake za msimu huu, huku wakitarajia kumchukulia hatua
kali zaidi juu ya ishara ya ubaguzi wa rangi aliyoionesha jana.
“Villarreal inaitangazia dunia kuwa imekerwa sana na kuchukizwa na
kitendo kilichotokea jana kwenye mechi dhidi ya FC Barcelona ambapo
shabiki alirusha ndizi katika uwanja El Madrigal”. Taarifa ya klabu
imesomeka.
“Shukurani kwa maafisa usalama na mashabiki wote. Klabu imefanikiwa
kumbaini shabiki huyo na kuamua kufuta tiketi zake za msimu huu na
kumfungia kifungo cha kudumu kutoingia katika uwanja wa El Madrigal”
“Kwa mara nyingine tena, klabu inapenda kueleza msimamo wake juu ya
heshima, usawa, undugu na mchezo wa kiungwana ndani na nje ya uwanja na
haitavumilia uvunjifu wa kanuni hizi kama vile kuleta fujo na ubaguzi
wa rangi”.
Kitendo alichofanyiwa Alves jana kimemkera Mbrazil mwenzake
aliyeweka picha katika mitandao ya kijamii akila ndizi kama ishara ya
kumuunga mkono kaka yake huyo mweye miaka 30 na kuandika maneno chini ya
picha yaliyosema: “Sisi wote ni nyani”.
Mabao mawili ya kujifunga na lile la Lionel Messi yaliwafanya Barca
kwa mbali waanze kufufua matumaini ya kutwaa ubingwa katika wiki hii
ngumu ambayo wamempoteza kocha wao wa zamani, Tito Vilanova
0 comments:
Post a Comment