Mechi
ya watani wa jadi Simba na Yanga ambayo ilichezwa April 19 imeingia
kwenye headline baada ya kuhusishwa na imani za kishirikina na hii ni
baada ya kufukuliwa kwa mayai 3 uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.
Urio ambaye ni Meneja wa Uwanja wa taifa amepatikana kulizungumzia
hili ameanza kwa kusema>>’Unajua mambo yanayohusiana na mambo ya
kishirikina kwanza Serikali haiyaamini,wanaozungumza mambo ya
kishirikina siwezi kuwakataza kuzungumza kwa sababu kila mtu ana imani
yake lakini sisi vitu hivyo hatujihusishi,hatuvutaki na hatutojihusisha
nayo kabisa kwa sababu hayako kwenye imani zetu na sio sehemu ya kazi’
‘Ni uongo kabisa vitu vifukuliwe uwanjani kama waliona na kama mtu
aliingia nalo yai huwezi kumwambia mtu hakukaguliwa kwa sababu yai hata
ukipita kwenye vile ving’amuzi vya polisi haviwezi kung’amua kwa sababu
yai sio chuma hivyo haviwezi kupiga kelele lakini hiyo mimi siwezi
kuelezea kwa sababu sijasikia mambo ya mayai wala kusikia sijaona vitu
vya uchawi lakini nimesikia watu wanazungumza’
‘Hii ipo kwenye michezo yote unayaikia ooh wameroga hawa wamefanya
hivi na huwezi kuwazuia watu kusema kwenye uwanja mpya wa Taifa
haijawahi kutokea’.
0 comments:
Post a Comment