Tishio
la kigaidi lina kodolea macho taifa la Kenya baada ya kundi la kigaidi
lililo na makao yake makuu nchini Somalia kuachia video nyingine kwenye
mtandao wa Al-Kataib wakitishia kutekeleza mashambulizi nchini Kenya
wakati wowote.
kwenye kanda hiyo msemaji wa alshabaab aliye jifunika uso anasema
kwamba hawaoni lolote litakalo wa zuia kuingia Kenya hasa baada ya
kufanikiwa kutekeleza mauaji katika jengo la west Gate. mwaka
uliopita>>’tumekuwa tukisema tutafika Kenya lakini hivi tayari
tushafika si eti westgate ndio tosha bado kuna mamia na mamia ya watu
wanaongojewa mahala kama hiyo insha Allah’alisema msemaji huyo.
Huku wakiimbia tutawalipua hadi tuwamalize wanamgambo hao wamesema
kwamba wameamua kuungana na wasomali kutetea dini ya Allah,Wadadisi wa
maswala ya kiusalama wanahoji kwamba huenda hawa ni baadhi ya vijana
kutoka kwa mataifa ya Afrika mashariki walipewa mafunzo ya itikadi kali
na baadaye kupelekwa somalia kujiunga na Alshabaab kutokana na
wanavyozungumza lugha ya Kiswahili kwa ufasaha kwenye video hiyo.
Ispekta mkuu wa polisi nchini Kenya bwana David kimaiyo amesema
uchunguzi umeanzishwa kubaini chanzo cha video hiyo na taarifa kamili
kutolewa punde tu watakapo pata habari zaidi kuhusiana na video hiyo.
0 comments:
Post a Comment