Mahakama moja nchini Misri
imewahukumu wafuasi 11 wa aliyekuwa rais wa taifa hilo Mohammed Morsi
kifungo cha kati ya miaka mitano hadi minane jela kwa kufanya
maandamano.
Washtakiwa hao walikamatwa kufuatia msururu wa
ghasia zilizozuka baada ya kundolewa madarakani kwa Mohammed Morsi mwaka
uliopita.Mnamo mwezi Machi, zaidi ya wafuasi 500 wa Mohammed Morsi walihukumiwa kifo katika mahakama hiyo hiyo.
kesi hiyo inajiri wakati ambapo kuna msako dhidi ya waislamu wenye itikadi kali wanaomuunga mkono Mohammed Morsi.
0 comments:
Post a Comment