Mapigano ya kugombea ardhi kati ya wakulima na wafugaji katika eneo la mpaka kati ya wilaya za Kishapu mkoani Sninyanga na Igunga, mkoani Tabora yameua watu watano.
Mapigano
hayo yaliyotokea Jumapili iliyopita katika kijiji cha Magalata wilayani
Kishapu na kusababisha vifo hivyo na mtu mmoja kujeruhiwa baada ya
kushambuliana kwa kutumia mikuki.
Waliouawa
ni Peter Korongo Masolwa(72) Chawalwa Duke(50) Diblo Kingu(50) Mohamed
msengi(40) Kende Doma(70) wakazi wa Kishapu na Igunga.
Mkuu
wa wilaya ya Kishapu, Wilison Nkhambaku, alisema mapigano hayo
yalitokea eneo la Magogo na kwamba wafugaji wa jamii ya Kitaturu
walinyang’anywa na wakulima mifugo yao zaidi ya ng’ombe 3,000 ambazo
ziliswagwa na kupelekwa wilayani Igunga.
Vita kati ya Wafugaji na Wakulima
Nkhambaku
alisema kutokana na tukio hilo, ilibidi kamati ya ulinzi na usalama wa
wilaya zote mbili Kishapu na Igunga walikaa kikao na kulijadili suala
hilo kwa kulitafutia ufumbuzi, na kuwa waliwataka wafugaji na wakulima
kuacha mapigano hayo ikiwa serikali inalitafutia ufumbuzi pamoja na
kutenga maeneo ya kilimo na sehemu za machungo ya mifugo.
Baadhi
ya wafugaji walisema mapigano hayo yalitokana na wakulima kulima mazao
maeneo yote na kusababisha kukosa maeneo ya malisho, hivyo kuamua
kutafuta haki yao kwa nguvu.
Mmoja
wa wafugaji hao, Ndelanha Mahona, alisema ng’ombe zaidi ya 3,000
waliswagwa na kupelekwa Igunga, kitendo ambacho wafugaji hawakukubali na
kusababisha mapigano hayo.
Wakulima
walidai wafugaji hao wamekuwa wakipitisha mifugo yao katika mashamba na
kulisha mazao yao, kitendo ambacho hawakukubaliana nacho kwa
kuwasababishia hasara kila mwaka.
Mwenyekiti
wa Halmashauri ya Kishapu, Justin Sheka, alisema mapigano hayo
yamehatarisha amani kwa wananchi, huku akiwataja walionyang’anywa
mifugo hiyo kuwa ni Ndelanha Mahona, Mbuta Madila, Silag’wan Hendeka,
Gidi Babashi na Gilijisiji Gilawida ambaye alijeruhiwa kwa kuchomwa
mkuki.
Mwenyekiti
wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kishapu, Shija Ntelezu,
aliitaka serikali kulitafutia ufumbuzi suala hilo haraka kutokana na
wananchi kuanza kuuana hovyo.
“Suala
hili linahitaji ufumbuzi wa haraka, eneo hilo la Mbuga ya Magalata
lilitengwa kwa ajiri ya machungio ya mifugo, lakini wakulima wamevamia
eneo hilo wakidai na wao wana haki ya ardhi na kuanza kulima mazao,
hivyo serikali haina budi kulitatua tatizo hilo haraka ili kuepusha
mauaji,” alisema Ntelezu.
Kufuatia mapigano hayo, wakuu wa mikoa ya Tabora na Shinyanga wameunda timu ya watu 18 kuchunguza chanzo cha mgogoro huo.
Mkuu
wa Mkoa wa Shinyanga, Ally Nasoro Rufunga na Mkuu wa Mkoa wa Tabora,
Fatuma Mwasa, walisema wameazimia kuwa wafugaji wa Kishapu wabaki katika
eneo lao la Magalata wasivuke mto Manonga.
Walisema
pia kwamba wakulima wa Igunga walioko katika vijiji vya Magogo na
Isakamaliwa wabaki katika vijiji vyao na wasivuke mto Manonga.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Shinyanga, Evarist Mangala, alisema msako unaendelea kuwabaini waliohusika na mapigano hayo
gumzolajiji
0 comments:
Post a Comment