JUMUIYA ya Marastafarian Tanzania, (Taramo), imeandaa Tamasha la kumbukumbu ya muasisi wa muziki wa Reggae ulimwenguni, Nesta Robert, maarufu kama Bob Marley litakalofanyika ufukwe wa hoteli ya Mbalamwezi jijini Dar es Salaam, leo.
Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Ras Bumijah alisema, tamasha hilo
limeandaliwa kwa ajili ya kuenzi mchango wa muasisi huyo, aliyechangia
pia kulinda mila na utamaduni wa marastararian ulimwenguni kote.
Alisema, kutokana na mchango wake huo, Jumuiya imekuwa ikifanya kumbukumbu kila mwaka na safari hii wamealika wasanii na wanamuziki wengi kwa ajili ya kutumbuiza katika tamasha hilo.
Ras Bumijah, aliwataja baadhi ya wasanii na wanamuziki watakaopamba
leo kuwa ni washindi wa tuzo za muziki za Kilimanjaro, Chibwa na Dabo,
Ras Mizizi, Man Kifimbo na yeye mwenyewe.
"Tumewaalika Dabo na Chibwa kuja, kutokana na kuutendea haki muziki huu ulioasisiwa na Bob Marley,
ambaye Jumamosi hii tunamkumbuka. Wataitumia nafasi hii kuwashukuru
wale wote waliofanikisha ushindi wao na wataimba live kwa ajili ya
mashabiki na wapenzi wa miondoko ya reggae," alisema Ras Bumijah.
Aliongeza kuwa, pamoja na wasanii hao kutoa burudani, pia kutakuwa
na burudani nyingine ya vikundi mbalimbali vinavyopiga muziki wa reggae
asili, sambamba na uuzaji wa mavazi ya asili ya kiafrika kama njia ya
kumuenzi Hayati Bob Marley.
0 comments:
Post a Comment