pagead2.googlesyndication.com pagead2.googlesyndication.com

Majambazi waua,wapora Sh milioni 20,Arusha

maja2
WATU wawili wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wakiwa na silaha aina ya Short gun wamepora kiasi cha Sh milioni 20 kutoka kwa mtumishi wa duka la kubadilishia fedha za kigeni la Northern Bureau de Change na kumpiga risasi mtu mmoja na kufa papo hapo.

Tukio hilo lililotokea saa 3.30 asubuhi jana katika duka hilo mali ya Hotel ya Impala lililopo mtaa wa Maeda katikati ya Jiji la Arusha.

Watuhumiwa hao wakiwa na pikipiki waliondoka eneo hilo kupitia barabara ya zamani ya Moshi kuelekea Kijenge mara baada ya tukio hilo.
maj2

Kwa mujibu wa watu walioshuhudia tukio hilo, walisema majambazi hao walifika eneo hilo na pikipiki na kuegesha eneo zinapoegeshwa teksi na kumsubiri mtumishi wa duka hilo aliyetambuliwa kwa jina moja la Mama Msuya ambaye jana aliingia kazini na usafiri mwingine tofauti na unaojulikana.

Mmoja wa watu hao ambaye hakuwa tayari kusema jina lake, aliendelea kusema mara baada mtumishi huyo kufika akiwa na mfuko mweusi wenye kiasi hicho cha fedha, ghafla alivamiwa mlangoni wakati akiwa anafungua duka hilo na kuanza kunyang’anyana mfuko huo.
maj3

Alisema wakati jambazi huyo mmoja akipambana na Mama Msuya na kumpiga kibao huku akimuamurisha kutoa fuko hilo la fedha, mama huyo alipiga kelele kuomba msaada na madereva teksi walikwenda haraka kutaka kumsaidia.

Lakini hali ilibadilika baada ya jambazi mwingine aliyebaki katika pikipiki kuteremka na silaha na kwenda kumpiga risasi mmoja wa watu aliyetaka kwenda kutoa msaada aliyetambuliwa kwa jina mmoja la Mmasi ambaye ni mchimba madini ya tanzanite na kufa papo hapo.
Mtoa habari huyo alisema Mmasi alikuwa ametoka kusali katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Mjini Kati na alikwenda kununua magazeti eneo hilo na alipoona mama akipiga kelele kuomba msaada, alikwenda kwa lengo la kumuokoa lakini kabla ya kufika alipigwa risasi ubavuni na kufa papo hapo na jambazi aliyekuwa pembeni na Toyo

0 comments:

Post a Comment