pagead2.googlesyndication.com pagead2.googlesyndication.com

Kwa wale waliopotelewa na VYETI Maelezo ya kupata kingine haya hapa

                                                 BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA
FOMU YA OMBI LA CHETI MBADALA (REPLACEMENT CERTIFICATE)  
A. SOMA MAELEKEZO YAFUATAYO KABLA YA KUJAZA FOMU HII. 
(i) Hakikisha kwamba taarifa utakazoandika katika fomu hii ni sahihi. Iwapo tarifa uliyoandika haitakuwa sahihi, cheti mbadala hakitaandaliwa. 
(ii) Gharama ya cheti mbadala ni Tsh. 100,000/=. 
(iii) Ombi la cheti mbadala litapokelewa baada ya miezi mitatu (03) kupita tangu kutangazwa gazetini kwa upotevu wa cheti cha awali. 
(iv) Mchakato wa uchunguzi utafanyika katika kipindi cha siku thelathini (mwezi mmoja) tangu kupokelewa kwa ombi la cheti mbadala ambapo Jeshi la Polisi (kitengo cha uchunguzi wa picha) litahusika katika kukamilisha uchunguzi huo. 
(v) Cheti mbadala kitatolewa mara moja tu. 
(vi) Iwapo cheti kilichopotea kitabainika kutumika katika soko la ajira au mafunzo na mtahiniwa akabainika kushiriki katika kulidanganya Baraza la Mitihani katika kumwezesha mtumiaji wa cheti hicho kukitumia wakati sio chake, hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi ya watu wote waliohusika katika udanganyifu huo. 
(vii) Hakikisha kwamba unavyo viambatisho vifuatavyo:
PICHA YA MTAHINIWA

Tangazo la gazeti la upotevu wa cheti (taarifa muhimu kwenye tangazo hilo ni Jina la mtahiniwa, Namba ya mtihani, aina ya mtihani, mwaka wa mtihani, jina la shule, picha ya mtahiniwa na mahali cheti kilikopotea), Hati ya polisi ya upotevu wa cheti, Picha (Passport size) utakayobandika kwenye fomu ya ombi la cheti mbadala, Nakala ya kitambulisho na Risiti halisi ya malipo. 
Iwapo cheti chako kiliungua moto, kuharibiwa na mchwa, mafuriko, panya au kwa namna nyingine yoyote hutatakiwa kutangaza gazetini uharibifu huo bali utawasilisha vielelezo vilivyotajwa hapo juu pamoja na barua ya serikali ya mtaa wa eneo la tukio la moto au mafuriko yalipotokea. Iwapo yapo mabaki ya cheti husika utatakiwa kuwasilisha mabaki hayo Baraza la Mitihani.  
(viii) Baada ya kukamilisha ujazaji wa fomu na malipo, tafadhali tuma au wasilisha fomu yenye viambatisho vilivyotajwa kwa Katibu Mtendaji, Baraza la Mitihani la Tanzania, S.L.P 2624 Dar es Salaam. Fomu hii inapatikana  katika tovuti ya Baraza ambayo ni:www.necta.go.tz  
Iwapo cheti kitatumwa kwa EMS, utapaswa kuongeza malipo kwenye gharama iliyotajwa kadri utavyoelekezwa na posta. 
Malipo yafanyike kwenye mojawapo ya akaunti za NECTA zifuatazo: 
 NBC  11103001074 BANK CORPORATE BRANCH 
 NMB  2011100238 NMB BANK-BANK HOUSE  
 CRDB 01J1013540000 CRDB BANK-TAWI LA  KIJITONYAMA.     

B. MASHARTI YA KUOMBA CHETI MBADALA 
Mwombaji wa cheti mbadala unatakiwa kutimiza masharti yafuatayo: 
(a) Uwe ni mtahiniwa halisi uliyefanya mtihani na kutunukiwa cheti cha awali chenye picha kisha kikapotea, kuharibika au kuungua moto. 
(b) Uwe mkweli, mwaminifu na mwenye dhamira ya kweli ya hitaji la cheti mbadala baada ya kutokuwa na cheti cha awali kwa sababu ya matukio yaliyotajwa katika kipengele (a) hapo juu. 
(c) Picha yako itafananishwa na picha iliyotumika kufanya mtihani husika. Iwapo picha hizo hazitafanana, uchunguzi utafanyika ili kubaini ukweli wa tofauti hizo. Aidha, iwapo matokeo ya uchunguzi yatabaini kuwa aliyefanya  mtihani huo ni mtahiniwa tofauti na wewe, basi itakuwa imethibitika kuwa ulikuwa unajaribu kujipatia cheti mbadala isivyo halali kinyume cha sheria. Hivyo, hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yako. 
(d) Cheti mbadala kitatumiwa na mtahiniwa husika tu katika ajira na mafunzo. Iwapo cheti kilichopotea (kwa waliopoteza vyeti) kitapatikana, cheti mbadala kirudishwe Baraza la Mitihani mara moja. 
(e) Uwe umetekeleza maelekezo yote yaliyoainishwa katika vipengele (i)-(iv) hapo juu.  
4  
C. KIAPO Mimi …………………………………………….. nathibitisha kwamba taarifa  nilizojaza katika fomu hii ni sahihi. Aidha, nitatekeleza masharti yote ya matumizi ya cheti mbadala kama yalivyoainishwa katika fomu hii. Iwapo nitabainika kuwa sikutoa taarifa sahihi na nikashindwa kutekeleza masharti ya matumizi ya cheti mbadala nichukuliwe hatua za kisheria. 
Saini:…………………………………Tarehe:…………………………………. 
D. TAARIFA ZA MTAHINIWA: 
(a) Jina kamili lililotumika katika mtihani …………………………... 
………………………………………………………………………………. 
(b) Aina ya mtihani aliofanya (CSEE, ACSEE, GATCE, GATSCCE, DEE/DSEE, DTE, FTC, ADE) …………………………………..…… 
(c) Mwaka wa mtihani ……………………………………………………. 
(d) Namba ya mtihani ……………………………………………………. 
(e) Anwani …………………………………………………………………… 
(f) Simu ……………………………………………………………………… 
(g) Barua pepe……………………………………………………………… 
Cheti mbadala kitakabidhiwa au kutumwa kwa mtahiniwa husika tu. Mwakilishi hataweza kupewa cheti hicho. 
i. Kiasi cha fedha iliyolipwa ni Tshs………………..….……..  
Saini…………………………. Tarehe………….……………  
ii. Cheti Mbadala kitumwe kwenye anwani ifuatayo au nikabidhiwe (jaza kipengele unachotaka kitumike): 
……………………………………………………………………

E. KWA MATUMIZI YA OFISI TU. 
(i) Nathibitisha kupokea ombi hili na/pasipo viambatanisho vilivyotajwa:  
Jina…………………………….Saini…………Tarehe ……………… 
(ii) Ombi limeshughulikiwa/halijashughulikiwa kwasababu ……………………………………………………………………………… 
Jina:……………………………….Saini:…………Tarehe: ……….… 

1 comments:

  1. Do you need to increase your credit score?
    Do you intend to upgrade your school grade?
    Do you want to hack your cheating spouse Email, whatsapp, Facebook, instagram or any social network?
    Do you need any information concerning any database.
    Do you need to retrieve deleted files?
    Do you need to clear your criminal records or DMV?
    Do you want to remove any site or link from any blog?
    you should contact this hacker, he is reliable and good at the hack jobs..
    contact : cybergoldenhacker at gmail dot com

    ReplyDelete