SAIDI
Mkutano
wa kitaalamu ambao unawakutanisha wataalamu mbalimbali kutoka tasnia za
mipango, uchumi, takwimu na maendeleo, wenye wajibu wa kusimamia uchumi na
mipango umefunguliwa rasmi na kuwakutanisha kwa pamoja wakurugenzi wa sera na mipango,
maafisa mipango kutoka kwenye wizara, Serikali za Mitaa, idara na wakala wa
Serikali, pamoja na taasisi za kitaaluma na watafiti wanaojishughulisha na
masuala ya maendeleo na uchumi.
Akizungumza
wakati wa ufunguzi wa mkutano huo, Balozi (Mstaafu) Dkt. Lumbanga alisema kuwa wachumi
na maafisa mipango wana wajibu mkubwa katika kuishauri serikali juu ya njia bora
na madhubuti za kupambana na umaskini na kuharakisha maendeleo kwa jamii ya
Watanzania.
“Muna dhima kubwa katika kushauri
kitaalamu juu ya namna nzuri za kupunguza tatizo sugu la umaskini miongoni mwa
Watanzania,” alisema.
Balozi (Mstaafu) Dkt. Lumbanga aliwasihi washiriki kutumia fursa hiyo
kujadili kwa kina na kubadilishana uzoefu juu ya sera, mipango na kujenga
mtandao wa masuala ya maendeleo ya kitaaluma.
Akizungumza
wakati wa ufunguzi wa Mkutano huo, Katibu Mtendaji wa Ofisi ya Rais,
Tume ya Mipango, Dkt. Philip Mpango alisema kuwa lengo kuu la mkutano huo ni kutoa fursa ya kuwakutanisha kwa pamoja
wataalamu hao na kujenga uelewa wa pamoja juu ya uendeshaji wa shughuli
mbalimbali za Serikali.
Aliongeza
kuwa Mkutano huo, unatoa fursa za kujadiliana kwa pamoja juu ya mafanikio na
njia za kukabiliana na changamoto kwa kubadilishana uzoefu na ujuzi kwenye
masuala hayo.
“Mkutano
huu ni muhimu katika kuimarisha utendaji kazi wa kada hizi kwa minajili ya
kusukuma gurudumu la maendeleo ya kiuchumi na kijamii nchini,” alisema Dkt.
Mpango.
Kwa
mujibu wa ratiba ya mkutano huo, Mada mbalimbali zinawasilishwa kwa kutilia
mkazo masuala mbalimbali ya kimaendeleo yanayojitokeza hivi sasa, ambapo mkutano
huo unajadili masuala ya Maendeleo ya Tasnia ya Wapanga Mipango (wachumi,
maafisa mipango na watakwimu) na Maandalizi ya Mpango wa Pili wa Maendeleo wa
Miaka Mitano (2015/16 – 2020/2021).
Mada
nyingine ni pamoja na Mwongozo wa Usimamizi wa Uwekezaji katika Sekta ya Umma
ambao una lengo likiwa kuimarisha utendaji, ufanisi na uwajibikaji katika
matumizi ya rasilimali za umma zilizotengwa kwa ajili ya miradi na program za
maendeleo. Pamoja na mada ya Namna bora ya kujiandaa na Uchumi wa Gesi.
Washiriki
wa mkutano huu ni pamoja na wakurugenzi wa sera na mipango, maafisa mipango
kutoka kwenye wizara, Serikali za Mitaa, idara na wakala wa Serikali, pamoja na
taasisi za kitaaluma na watafiti wanaojishughulisha na masuala ya maendeleo na
uchumi.
Katibu Mtendaji wa Ofisi ya Rais,
Tume ya Mipango, Dkt. Philip Mpango akisoma hotuba wakati wa mkutano wa mwaka
wa wachumi na maafisa mipango unaofanyika jijini Dar es Salaam.
Mgeni Rasmi wa mkutano wa mwaka wa
wachumi na maafisa mipango, Balozi Dkt. Matern Lumbanga akizungumza na
washiriki wa Mkutano huo kabla ya kuufungua rasmi.
Katibu Mtendaji wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Dkt.
Philip Mpango (Kulia) akimpongeza na kumshukuru Mgeni Rasmi wa mkutano wa mwaka
wa wachumi na maafisa mipango, Balozi Dkt. Matern Lumbanga mara baada ya
kuufungua rasmi mkutano huo.
Baadhi ya viongozi wa wa Ofisi ya
Rais, Tume ya Mipango wakimsikiliza kwa makini Katibu Mtendaji wa Ofisi ya
Rais, Tume ya Mipango, Dkt. Philip Mpango (Hayupo pichani). Kutoka Kushoto ni
Naibu Katibu Mtendaji (Uchumi Jumla), Prof. Longinus Rutasitara, anayemfuatia
ni Bw. Paul Sangawe (Naibu Katibu Mtendaji anayeshughulikia Biashara za
Kimataifa na Mahusiano ya Kiuchumi) na Kulia ni Naibu Katibu Mtendaji (Huduma
za Jamii na Masuala ya Idadi ya Watu) Bibi Florence Mwanri.
Washiriki wa mkutano wa mwaka wa wachumi na maafisa mipango
wakimsikiliza Katibu Mtendaji wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Dkt. Philip
Mpango (Hayupo pichani).
Washiriki wa mkutano wa mwaka wa
wachumi na maafisa mipango wakiwa katika picha ya pamoja na Mgeni Rasmi Balozi
Dkt. Matern Lumbanga (katikati waliokaa) pamoja na viongozi waandamizi wa Ofisi
ya Rais, Tume ya Mipango.
Picha
na SAIDI MKABAKULI
0 comments:
Post a Comment