MWANRI: ZINGATIENI WELEDI WAKATI
WA KUANDAA MAANDIKO YA MIRADI
Na
Saidi Mkabakuli
Wapanga
mipango nchini wameaswa kuzingatia weledi wakati wa kuandaa maandiko ya miradi
yanayowasilishwa kwa wafadhili ili kuongeza ushindani dhidi ya nchi nyingine
wakati wa uwasilishaji wa maombi ya kupatiwa ufadhili wa miradi ya maendeleo.
Wito
huo umetolewa na Kaimu Katibu Mtendaji wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi
Florence Mwanri wakati alipofanya mazungumzo na viongozi waandamizi kutoka wizara
za viwanda na biashara, fedha, uchukuzi, nishati na madini pamoja na viongozi
waandamizi kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Zanzibar.
Bibi
Mwanri alisema kuwa kuna ushindani mkubwa kwa nchi zinazoomba ufadhili wa
miradi ya maendeleo hivyo uandishi wa maandiko yenye kuzingatia weledi na
viwango vya kimataifa ni msingi katika kuongeza ushindani na kuweza
kuwashawishi wafadhili kuvutiwa na miradi husika.
“Katika
kukabiliana na ushindani hatuna budi kujikita katika weledi na kuandika
maandiko yenye kuweza kuvutia wafadhili ili waweze kuja kuwekeza nchini kwetu,
ili tuweze kutimiza ndoto zetu za kuifanya Tanzania kuwa nchi yenye uchumi wa
kati kufikia mwaka 2025” alisema Bibi Mwanri.
Mwezi
Juni mwaka 2011, Serikali iliandaa Mpango wa Kwanza wa Maeneleo (2011/12 –
2015/16) kwa lengo la kutekeleza Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 ambapo Mpango
huu ulihitaji takribani trilioni 40 ili kutekeleza miradi mbali mbali ya
maendeleo kwa kipindi cha miaka mitano.
Kwa
mujibu wa Mpango huo, vyanzo vya utekelezaji wake ni pamoja na Ubia Kati ya Sekta ya Umma na Sekta
Binafsi (PPP); uwekezaji wa kigeni; Hati
Fungani kwa Waishio Ughaibuni; Hatifungani za ndani; Hati Fungani katika Masoko
ya Nje; Mifuko ya Pensheni na hifadhi ya jamii; na makubaliano ya ushirikiano
wa kiuchumi wa nchi zinazoendelea.
Kaimu Katibu Mtendaji
wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (aliyesimama) akizungumza
na baadhi ya viongozi waandamizi wizara za viwanda na biashara, fedha, uchukuzi,
nishati na madini pamoja na viongozi waandamizi kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya
Mipango, Zanzibar.
Bibi Maryam Khamis
(Wapili kulia) Mtaalam wa uchumi kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango,
Zanzibar akizungumza katika kikao hicho.
Pichani ni baadhi ya
viongozi waliohudhuria Kikao hicho. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya
Ukanda Maalumu wa Uwekezaji nchini (EPZA), Dkt. Adelhelm Meru.
Mmoja wa wajumbe wa
kikao hicho, Bw. Aunyisa Meena kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara akichangia
mada.
0 comments:
Post a Comment