TANZANIA
YAJIPANGA KUWA NCHI YA VIWANDA
Na
Saidi Mkabakuli
Serikali imesema imedhamiria
kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda ifikapo mwaka wa fedha 206/2017 ili
kuongeza kasi ya kufikia lengo la Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 ambayo imedhamiria
kuifikisha Tanzania kuwa nchi yenye hadhi ya kipato cha kati na kuondokana na
umaskini kufikia mwaka 2025.
Akizungumza wakati wa
kuwakaribisha Ugeni kutoka Tume ya Mipango na Maendeleo ya China, Naibu Katibu
Mtendaji anayeshughulikia Biashara za Kimataifa na Mahusiano ya Kiuchumi, Bw.
Paul Sangawe, amesema kuwa Tanzania imedhamiria kuaandaa Mpango wa miaka mitano
utakaojikita katika uchumi wa viwanda ndani ya muda mfupi ujao.
“Tumedhamiria kuwekeza nguvu
zetu kwenye uwekezaji katika viwanda; katika Mpango wa Pili wa Maendeleo, nguvu
kubwa tunaiweka katika maendeleo ya viwanda ili kuweza kufikia malengo ya Dira
ya Taifa ya Maendeleo 2025,” alisema Bw. Sangawe.
Akizungumza wakati wa kikao cha
pamoja na viongozi wa Tume ya Mipango ya Tanzania, Kiongozi wa Msafara huo, Bw.
Wang Jianjun ambaye ni Naibu Mkurugenzi Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji,
alisema kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi chache barani Afrika zenye fursa
kubwa ya kufikia maendeleo na kuweza kuondoka kwenye kundi la nchi maskini
ndani ya kipindi kifupi kijacho.
Bw. Jianjun aliongeza “ili
kuweza kufikia maendeleo ya haraka zaidi, ni vyema Tanzania ikaanza kuwekeza
katika viwanda hasa kwenye Maeneo Maalum ya Kiuchumi (SEZs) ili kuongeza tija
katika uzalishaji na kuongeza thamani bidhaa zake ili kuvutia masoko toka nje
ya nchi.”
Naibu Katibu Mtendaji (Uchumi
Jumla), Prof. Longinus Rutasitara (Wapili kushoto) akizungumza na Ugeni kutoka
Tume ya Mipango na Maendeleo ya China wakati walipofanya ziara nchini. Kushoto
ni Naibu Katibu Mtendaji (Biashara za Kimataifa na Mahusiano ya Kiuchumi), Bw.
Paul Sangawe.
Naibu Katibu Mtendaji (Biashara
za Kimataifa na Mahusiano ya Kiuchumi), Bw. Paul Sangawe akizungumza wakati wa
ziara hiyo. Kushoto ni Kaimu Katibu Mtendaji wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango,
Bibi Florence Mwanri.
Kiongozi wa Msafara huo, Bw. Wang
Jianjun (Aliyesimama) ambaye ni Naibu Mkurugenzi Mkuu anayeshughulikia
Uwekezaji kutoka Tume ya Mipango na Maendeleo ya China akizungumza wakati wa
ziara hiyo.
Naibu Katibu Mtendaji (Biashara
za Kimataifa na Mahusiano ya Kiuchumi), Bw. Paul Sangawe akiwasilisha Mada ya Hali ya Uchumi wa Tanzania wakati Ugeni kutoka Tume ya Mipango na
Maendeleo ya China wakati walipofanya ziara nchini.
Ugeni kutoka Tume ya Mipango na
Maendeleo ya China wakifuatilia kwa makini nyaraka mbalimbali walipotembelea
Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango.
Naibu Katibu Mtendaji (Uchumi
Jumla), Prof. Longinus Rutasitara (kushoto) akimkabidhi zawadi Kiongozi wa
Msafara huo, Bw. Wang Jianjun (kulia).
Picha ya pamoja: Ugeni kutoka
Tume ya Mipango na Maendeleo ya China wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi
ya viongozi waandamizi kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango na maafisa
waandamizi kutoka wizara za viwanda na biashara, uchukuzi, nishati na madini
pamoja na viongozi waandamizi kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Zanzibar.
0 comments:
Post a Comment