Mwanamume ambaye kazi yake ni ya upishi nchini Australia, anadaiwa
kumuua mpenzi wake na kumkatakata vipande na kupika baadhi ya sehemu
zake za mwili.
Aliyafanya unyama huo kabla ya yeye mwenyewe kujitoa uhai wake.
Marcus Volke, mwenye umri wa miaka 28, alijikataa koo yake huku
akiwatoroka polisi waliokuwa wamekuja kufanya uchunguzi baada ya
majirani zake kuripoti kuwepo harufu mbaya mfano wa nyama iliyooza
iliyokuwa inatoka nyumbani kwa mwanamume huyo.
Maafisa wa polisi walipata sehemu za mwili wa mwanamke huyo zikitokota
kwenye sufuria iliyokuwa imejazwa kemikali huku vipande vingine vikiwa
kwenye karatasi za plastiki za takataka nje ya nyumba katika mtaa wa
kifahari za Teneriffe.
Taarifa hii ni kwa mujibu wa jarida la Brisbane Courier Mail. Mwanamke huyo raia wa Indonesia bado hatajambulishwa rasmi.
Wapenzi hao waliokuwa wanaishi pamoja walikutana wakiwa wanafanya kazi kwa meli za kifahari na wote walikuwa wameajiriwa.
Wakazi wa mtaa huo waliambia vyombo vya habari kuwa harufu mbaya ilikuwa
inatoka katika myumba ya Volke na ikazidi kuwa mbaya siku ziliposonga.
"nilipotoka nje harufu hiyo ilisababisha machozi kutoka machoni na hata
kunifanya kujihisi mgonjwa,'' alisema mkazi mmoja. ''Ungedhani chakula
cha Mbwa au nyama ilikuwa imeachwa nje kwa siku kadhaa.''
Polisi wangali wanafanya uchunguzi.
0 comments:
Post a Comment