Wananchi
wa kijiji cha Mfuto katika Kata ya Ufulumo huko Wilayani Uyui, Tabora
wamepatwa na mshituko na kuingiwa na hofu baada ya mti aina ya msufi,
uliong’oka na kuanguka miaka mitatu iliyopita, kuinuka na kusimama wima
kama zamani.
Mti
huo wenye kipeo cha futi mbili inaelezwa kuwa ulianguka kwa upepo mkali
na kuungua kwa moto wakati wa kuandaa mashamba. Mtangazaji wa TBC
anasema kuwa mti huo ambao ulikuwa umeshambuliwa na mchwa, hivi majuzi
ulionekana ukinyanyuka taratibu kana kwamba walikuwepo watu wanaunyanyua
hadi uliposimama kama awali.
Mara
baada ya kuenea kwa taarifa za kuinuka kwa mti huo, wananchi wengi
walifika kwenye eneo husika na kuanza kugombea vipande vya mti huo,
ambapo kila mtu alitaka kupata walao gome au sehemu yoyote ya mti huo
ama hata udongo palipokuwa pamelala mti huo.
Afisa
Mtendaji wa Kijii hicho, amesema kuwa Serikali ya Kijiji inaendelea
kuwasiliana na Wazee wa kimila ili kupata maoni yao juu ya tukio hilo
0 comments:
Post a Comment