Magenge ya uhalifu yanaendelea kuyalenga magari yasio na funguo.
Kulingana
na kundi moja la kampuni za magari nchini Uingereza,wezi hao huweza
kulemaza mfumo wa usalama wa magari hayo kupitia vifaa vinavyotumika na
fundi wa magari.
Hatahivyo watengezaji hao wa magari wanajaribu
kuwa mbele ya teknolojia inayotimiwa na wezi hao kwa kuimarisha
programmu inayotumika.
Imeripotiwa kuwa wamiliki kadhaa wa magari ya Range Rover nchini Uingereza wamenyimwa bima kutokana na swala hilo.
Na
huku umaarufu wa magari yasio na funguo ukiongezeka,wezi wamekuwa
wakinunua vifaa kupitia njia ya mitandao ambavyo vinaweza kuyafungua
magari hayo.
''Uhalifu wa kuiba magari kupitia utengezaji wa
rimoti zinazotumika kama funguo ni tatizo kubwa'', ilisema kampuni ya
Jaguar Land Rover.
''Hatahivyo tunalichukulia swala hilo na uzito
mkubwa huku timu yetu ya wahandisi wakiendelea kufanya kazi na kampuni
za bima na maafisa wa polisi ili kutatua swala hili''.
0 comments:
Post a Comment