Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Said Mwema.
Taarifa iliyotolewa na kuthibitishwa na Msemaji wa Polisi, Advera
Senso, imesema Kimea alifariki juzi na Jeshi la Polisi kwa kushirikiana
na familia ya marehemu imesafirisha mwili wa marehemu kwenda kijijini
kwao Mwera mkoani Tanga, kwa mazishi.
Senso alisema Jeshi la Polisi limepata pengo kubwa kwa kuondokewa
na kamishina huyo kwa kuwa alikuwa mtendaji hodari hali iliyomfanya
kutunukiwa nishani ya utumishi wa muda mrefu na Rais Jakaya Kikwete.
Alisema Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Said Mwema amezipokea
taarifa za kifo hicho kwa huzuni hasa ikizingatiwa hivi sasa askari
mmoja anahudumia watu takribani 1300 hadi 1500.
ACP Kimea alijiunga na Jeshi la Polisi Mwaka 1985 na kupandishwa
vyeo mbalimbali hadi kufikia cheo cha Kamishna Msaidizi wa Polisi ambapo
mpaka mauti yanamkuta alikuwa mkuu wa Kitengo cha Mipango ya
Raslimaliwatu, Makao Makuu ya Jeshi la Polisi na nafasi nyingine
alizowahi kushika ni pamoja na kuwa Mkuu wa Upelelezi wilayani Misungwi,
Mkuu wa Polisi wilayani Misungwi na Geita pamoja na Mnadhimu Mkuu wa
Polisi mkoani Morogoro.
chanzo Nipashe
0 comments:
Post a Comment