Meneja Uhusianio wa Tanesco, Badra Msoud.
Baadhi ya wananchi wameeleza kuwa pamoja na makao makuu ya shirika
hilo kueleza nguzo hakuna, lakini wapo wateja wengine hupatiwa nguzo kwa
njia zisizo halali.
Akizungumza na gazeti hili, Meneja Uhusianio wa Tanesco, Badra
Msoud, alisema upo uhaba mkubwa wa nguzo za umeme na kwamba zilizopo ni
kwa ajili ya dharura.
“Wateja wetu wasubiri kwa wiki mbili, kwani nguzo hizo ziko njiani
kutoka South Africa na nyingine zinatoka hapahapa nchini,” alisema.
Kampuni za ndani zilizoshinda zabuni ya kusambaza nguzo za Tanesco
ni Critical Engineering Solutions Construction Co, Sao Hill Industries
Ltd na Mufindi Wood Poles.
Kampuni za nje ni kutoka Afrika Kusini za Treated Timbers Products,
Low’s Treated Timbers (Ptg), Rousant International na Maghilika Timber
Ptg Ltd.
Badra alisema kuwa Tanesco inatumia sheria ya manunuzi na kwamba
kampuni zote zilishindanishwa kwa tenda na zilizoshinda zilitimiza
vigezo ikiwa ni pamoja na bei elekezi.
Kwa mujibu wa Badra, kabla ya nguzo kupokelewa na Tanesco,
hufanyiwa uchunguzi wa kina ikiwa ni pamoja na majaribio ya kiufundi ili
kuthibitisha ubora na kama zinakidhi viwango vya ubora vilivyoainishwa
kwenye zabuni ndipo hati za kuzipokea zinasainiwa.
chanzo Nipashe
0 comments:
Post a Comment