pagead2.googlesyndication.com pagead2.googlesyndication.com

VIONGOZI WA DINI WAPINGANA IRINGA

 
 Huyu  ndie  mhubiri maarufu  wa  kimataifa  kutoka Afrika ya kusini ambae  yupo kushusha neema ya maombi kwa wakazi wa mkoa  wa Iringa anaitwa nabii  Joshua Cyrill
 Mhubiri maarufu  kutoka nchini Kenya mtume Bonface Indeche ambae  pia amekuwa ngunzo kubwa mkoani Iringa kwa  huduma  yake  nzuri ya  kiroho anayoendelea  kuitoa

Kama  ni  vita mbaya ambayo  inaweza  kupoteza heshima ya  kiroho  mkoni Iringa ni pamoja na mbinu chafu zilizojitokeza  siku za hivi karibuni kwa baadhi ya  wahubiri  mkoani hapa  kuendekeza uchoyo  wa kihoro na  kutaka  kuendelea   kuhubiri wenyewe na sio wengine .
Uchunguzi  wa  kina  uliofanywa na mtandao  huu  wa  www.francisgodwin.blogspot.com umebaini  kuwepo kwa vita  kubwa kati ya baadhi ya  wahubiri  wa makanisa haya  yaliyoanza  kuchipuka  siku za hivi karibuni kwa  kuwazuia wahubiri  wengine kuifanya huduma  hiyo ndani ya  mkoa  wa Iringa.
Majina ya  wahubiri hao ambao  wanaendekeza  uchoyo  wa Kiroho kwa  sasa yamewekwa  kapuni na mtandao huu ,ila hali iliyofikiwa ni mbaya na iwapo suala   hili  litaendelea  kunyamaziwa  upo  uwezekano   mkubwa wa heshima na  sifa ya  viongozi wa  dini ikatoweka na waumini  wao kuanza kuhoji mengi juu ya hali  hiyo.
Mtandao huu  umekuwa ukifuatilia picha nzima ya vita  hiyo inayoendelea na  kuna njama zinazopangwa za kuendelea  kuwaharibia wahubiri hao japo  wakazi wa mjini  wa Iringa wametokea  kuwapongeza kwa ujio  wao ndani ya mkoa  wa Iringa wenye tatizo kubwa la UKIMWI na  kutaka  wahubiri  wenyeji wa makanisa  hayo  kuacha wivu wa huduma na badala  yake  kujipanga  upya na kuwapa ushirikiano wageni hao .
Wahubiri hao ambao  walipangwa  kuanza semina ya  neno ya Mungu kuanzia  Machi 21 mwaka  huu katika  ukumbi wa Embakasy Ilala   wamezuiwa  kufanya hivyo baada ya mhubiri  mmoja  kudaiwa  kutumika kuwavuruga  wahubiri  hao 
...........Usikose  kuendelea  kufuatilia undani wa  sakata  hili hapa

CHANZO: FRANCIS GODWIN

0 comments:

Post a Comment