Dar es Salaam: Tuzo za umahiri wa Uandishi wa
Habari Tanzania (EJAT) kwa mwaka 2012 zinatarajiwa kutolewa leo na
Baraza la Habari Tanzania (MCT), huku Waandishi wa Habari wa Magazeti ya
Mwananchi Communications Limited (MCL), wakitarajia kung’ara.
Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein ndiye atakayekabidhi tuzo ya mshindi wa jumla katika hafla hiyo itakayofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.
Hafla hiyo inatarajiwa kuhudhuriwa na waandishi pamoja na wadau mbalimbali wa habari nchini ili kushuhudia tukio hilo.
Waandishi wa Habari wa MCL inayochapisha magazeti ya Mwananchi, The Citizen na Mwanaspoti wanaotarajia kupanda jukwaani kuchukua zawadi ya jumla ni pamoja na Raymond Kaminyoge, Lucas Liganga, Florence Majani na Fred Azzah.
Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari, iliyotolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi wa Tuzo za EJAT 2012, Kajubi Mukajanga jumla ya kazi 946 ziliwasilishwa na waandishi kushindanishwa, idadi ambayo imetajwa kuwa ni kubwa ikilinganishwa na miaka mitatu iliyopita.Mukajanga aliwapongeza waandishi mbalimbali waliowasilisha kazi zao.
0 comments:
Post a Comment