Mke wake ndiye atamshikia Biblia na yeye atakuwa anaishika kwa kuweka mkono kama alivyofanya Rais Obama wa Marekani
Nairobi. Rais Mteule wa Kenya,
Uhuru Kenyatta amesema kwamba wakati wa kuapishwa hataapa kwa kuinua
Biblia bali atasaidiwa na mkewe kama alivyoapishwa Rais Obama wa
Marekani.
Mkuu wa Majeshi ya Kenya (KDF), Jenerali Julius Karangi alisema jana kuwa Kenyatta aliomba mkewe Margaret Kenyatta amshikie Biblia atakapokuwa akiapishwa.
Mkuu wa Majeshi ya Kenya (KDF), Jenerali Julius Karangi alisema jana kuwa Kenyatta aliomba mkewe Margaret Kenyatta amshikie Biblia atakapokuwa akiapishwa.
“Hili ni ombi la rais mteule na itakuwa vyema tukubali ombi lake katika siku hii ya kihistoria,” alisema Jenerali Karangi.
“Mke wangu atanishikia biblia kisha nitaweka mkono kama alivyofanya Omaba,hakuna Rais wa Kenya aliefanya hivyo” alisema
“Mke wangu atanishikia biblia kisha nitaweka mkono kama alivyofanya Omaba,hakuna Rais wa Kenya aliefanya hivyo” alisema
Kenyatta ataweka tu mkono wake wa kushoto juu ya
Biblia ikishikiliwa na mkewe, katika kile anachotaja hatua ya kuachana
na mtindo wa awali wa kuapisha marais wa Kenya wakiinua Biblia.
Kenyatta ataiga mfano wa Rais Barack Obama wa
Amerika, alipoapishwa hadharani mjini Washington DC mnamo Januari 21,
2013, ambapo aliomba mkewe Michelle Obama amshikie Biblia.
Siku hiyo Rais Mwai Kibaki atamkabidhi katiba mpya
Kenyatta, ambayo ilianza kutumika mnamo Agosti 2010. Mtindo huu utakuwa
wa kwanza tangu nchi hiyo kupata Uhuru. Sherehe hiyo itafanywa katika
Uwanja wa Michezo wa Moi Kasarani, ambapo pia Naibu wa Rais William Ruto
ataapishwa.
Shughuli hiyo inatarajiwa kumalizika saa 7.45. Kamati ya Mamlaka ya Ofisi ya Rais tayari ina ratiba ya mpangilio wa shughuli hiyo.
Ratiba hiyo ina picha ya rais anayeondoka katika ukurasa wa pili na ya Kenyatta katika ukurasa wa tatu. Kamati hiyo imeteua Rais Yoweri Museveni kuzungumza kwa niaba ya wageni wote waalikwa siku hiyo.

Hapo jana asubuhi, kamati hiyo inayoongozwa na
Mkuu wa Utumishi wa Umma, Francis Kimemia, ilisema kwamba shughuli
itaanza rasmi 5:45 asubuhi Rais Kibaki atakapowasili uwanjani.
Kulingana na mpangilio uliopo, wageni watahitajika
kusimama Rais Kibaki akiwasili, wakati wa sherehe ya kuapishwa, saluti
ya mizinga 21 itakapopigwa nje ya uwanja na wimbo wa taifa utakapoimbwa
kabla ya Rais Kibaki na rais mpya kuondoka uwanjani.
Siku hiyo, Kenyatta atapambwa kwa vifaa vya
mamlaka ambavyo ni pamoja na Mkuu wa Nakshi (CGH), pia atapokea mkuki,
ngao na katiba.
Zana hizo zinaashiria mamlaka; kwa mfano Katiba
inasimamia Kenya na watu wake, mkuki unasimamia Amiri Jeshi Mkuu ilhali
CGH ni heshima kubwa zaidi Kenya.
0 comments:
Post a Comment