Ni kuhusu tuhuma za Chadema kwa Waziri wa Uchukuzi , Dk Harrison Mwakyembe juu ya masuala ya TPA.
Dar es Salaam. Siku moja baada ya
Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Chadema kumtuhumu Waziri wa Uchukuzi
Dk Harrison Mwakyembe kwamba anakipendelea Chama Cha Mapinduzi (CCM),
chama hicho kimejibu mapigo kikidai kuwa Chadema kinahadaa wananchi na
hakina uhakika na kile wananchokizungumza.
Juzi, Mkurugenzi wa Oganaizesheni na Mafunzo, wa
Chadema, Benson Kigaila alisema Waziri Mwakyembe anatakiwa kuwaeleza
Watanzania juu ya uamuzi wa kuipa zabuni kampuni hiyo.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Katibu wa
Itikadi na Uenezi wa Chama hicho, Nape Nnauye alisema Kampuni ya
Jitegemee Trading Company ambayo inamilikiwa na Chama hicho haijaingia
mkataba na Mamlaka ya Bandari ( TPA) ili kutoa eneo lake la Sukita kwa
matumizi ya mamlaka hiyo kama walivyodai Chadema. Mbali na hilo chama
hicho kimesema viongozi wa Chadema wanapenda kuzungumza uongo na chuki.
Kauli hiyo ilitolewa jana ,baada ya Chadema
kumtuhumu Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe kikidai ametoa
zabuni ya upanuzi wa TPA kwa Kampuni ya Jitegemee Trading Company
kinyume cha utaratibu wa sheria za ununuzi.
Nape alisema kiwanja hicho, chenye ekari 100
kilichopo eneo Bonde la Mto Msimbazi, ambacho kinamilikiwa na Kampuni
ya CCM hakijaingia mkataba na Kampuni yoyote, licha ya kampuni zaidi ya
saba ambazo zimeomba zabuni ya kumiliki eneo hilo ikiwamo TPA.
‘‘Chadema ni waongo tena wanawapotosha Watanzania. Sisi tunaona kwamba wanapoelekea watapotea kabisa.’’
‘‘Chadema ni waongo tena wanawapotosha Watanzania. Sisi tunaona kwamba wanapoelekea watapotea kabisa.’’
MANANCHI
0 comments:
Post a Comment