Singida na Same.
WATU 13 wamefariki dunia papo hapo na wengine kadhaa kujeruhiwa
baada ya gari walilokuwa wakisafiria kutoka Itigi kwenda mkoani Singida
kupata ajali katika Kijiji cha Isuna, Wilaya ya Ikungi, mkoani hapa.
Akizungumza na Tanzania Daima jana kwa njia ya simu, Kamanda wa
Polisi wa Mkoa huo, Geofrey Kamwela, alisema kuwa ajali hiyo imetokea
eneo la Singida Kusini, mkoani humo.
Kamanda Kamwela alisema kuwa ajali hiyo ilihusisha gari namba T 730 BUX Noah, ambalo liligongana uso kwa uso na lori T 687 AXD Scania, lililobeba samaki likitokea jijini Mwanza.
Kamanda Kamwela alisema kuwa ajali hiyo imetokea saa 1:32 asubuhi kwenye barabara kuu ya Singida-Dodoma, ambapo kati ya maiti 13, watatu ni wa familia moja waliokuwa katika gari dogo aina ya Noah.
Alisema kati ya maiti hizo wawili ni wanawake na wanaume ni 11, huku abiria wengine watatu wakinusurika na kupata majeraha madogo madogo, ambapo wamekimbizwa katika hospitali ya mkoa huo.
Kamanda Kamwela alisema kuwa miili ya abiria 10 imetambuliwa na ndugu zao huku miili ya abiria watatu bado haijatambuliwa.
Aliwataja waliotambuliwa ni watu wa familia moja, Omari Shabani (44), mkewe Salma Omari na mtoto wao, Nyamumwi Omari (10), wote wakazi wa mji mdogo wa Itigi.
Wengine ni Haji Mohammed (29) (Msisi), Mtunku Rashidi (68) (Sajaranda), Salehe Hamisi (28) (Sajaranda), Samiri Shabani (20) (Puma), Mwaleki Nkuwi (35) (Ikungi), Athumani Kalemba (38) na Ramadhani Mkenga (Sajaranda).
Kamanda huyo alisema kuwa lori hilo lilipopishana na Noah lilihama kutoka upande wake na kuifuata Noah ambayo ilikuwa upande wake wa kushoto, hivyo kuligonga na kisha kuliburuza umbali wa zaidi ya mita 15.
“Bado hatujajua chanzo cha ajali hiyo mbaya, ingawa baadhi ya watu wanadai huenda dereva wa lori alisinzia, hivyo kusababisha lori hilo kuhama upande wake na kuifuata Noah na kwamba uchunguzi utakapokamilika tutatoa taarifa hiyo,” alisema.
Kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya mkoa huo, Dk. Deogratius Banuba, alikiri kupokea miili ya abiria hao 13 na kwamba kati yao miwili ni ya watoto.
Ajali hii imetokea ikiwa ni zaidi ya wiki moja tangu watu wenye hasira mkoani humo walichome moto basi la Kampuni ya Mtei Express, baada ya kugonga pikipiki iliyobeba watoto watatu wa familia moja na baba yao.
Katika tukio hilo, watoto watatu waliokuwa katika pikipiki hiyo walifariki dunia, huku abiria waliokuwa kwenye basi hilo hakuna aliyeumia wala kupoteza. maisha
Waliokufa katika ajali hiyo ni watoto Stamili Shabani (23) na Kassimu Shabani (19), ambao walikufa papo hapo, wakati Hamza Shabani (15), alifia katika hospitali ya mkoa wakati madaktari wakiendelea kuokoa maisha yake.
Huku baba mzazi wa watoto hao, Shabani Bunku (45), alidaiwa kuvunjika mguu na mkono wa kulia pamoja na kupata jeraha kubwa kichwani.
Kamanda wa Polisi mkoani humo, SACP Geofrey Kamwela, alisema wanafamilia hao walikuwa wakienda shamba kwa ajili ya palizi, ambapo basi lililohusika na ajali hiyo ni aina ya Scania, namba T 742 ACU.

Ajali Same
Katika tukio jingine, watu watatu wamepoteza
maisha na wengine zaidi ya 30 kujeruhiwa vibaya baada ya gari walilokuwa
wakisafiria kuacha njia na kupinduka katika Kijiji cha Mkwini, Barabara
Kuu ya Same – Mombo wilayani Same mkoani Kilimanjaro.
Gari hilo la Kampuni ya Hood lililokuwa likitokea
Iringa kuelekea Arusha lilianguka kati ya Makanya na Hedaru na
kusababisha vifo vya watu wawili papo hapo na mmoja alipoteza maisha
akiwa njiani akipelekwa hospitalini.
Mkuu wa Wilaya ya Same, Herman Kapufi alisema
ajali hiyo ilitokea juzi saa 11:45 jioni ikihusisha Basi la Hood
lililokuwa likiendeshwa na Baraka Juma ambaye alikimbia baada ya ajali
hiyo kutokea.
“Nilifika katika eneo la ajali, dakika 10 baada ya
gari kuanguka na tuliwatoa majeruhi 30 na wanaume wawili walikuwa
wamekufa papo hapo na tulipofika Hospitali ya Same alifariki majeruhi
mwingine na hivyo kufanya idadi ya waliokufa kufikia watatu,” alisema
Kapufi.
Alisema majeruhi 25 wanaendelea na matibabu katika
Hospitali ya Wilaya ya Same wakati majeruhi watatu walipelekwa katika
Hospitali ya Rufaa ya KCMC kutokana na hali zao kuwa mbaya na kwamba
miili ya marehemu imehifadhiwa katika Hospitali ya Same.
Kapufi alisema abiria walionusurika walisema kuwa
chanzo cha ajali hiyo kinaweza kuwa ni uchovu wa dereva, kwani basi
halikuwa kwenye mwendo kasi bali alionekana akiwa kwenye hali ya
kusinzia.
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Same, Dk Ernest Kyungu
alikiri kupokea majeruhi 30 na miili ya watu watatu ambao walipoteza
maisha na majeruhi watatu ambao hali zao ni mbaya walipelekwa Hospitali
ya Rufaa ya KCMC.
0 comments:
Post a Comment