Kiteto. Wafugaji 12 wa jamii ya
Kimasai wilayani Kiteto, katika Mkoa wa Manyara, wamefikishwa
mahakamani wakikabiliwa na kesi ya mauaji ya wakulima tisa.
Mwendesha Mashtaka Sajenti wa Polisi, Oscar
Munisi, alidai kuwa watuhumiwa walitenda makosa hayo Januari 12 mwaka
huu, katika Vitongoji cha Laitime na Mtanzania wilayani Kiteto.
Aliwataja watuhumiwa kuwa ni, Michael Lepunyati,
Richard Mlahangwa, Kipande Luguto, Lembris William, Meshack Ololipwa,
Zacharia Ololipwa, Mosonic Ngangwai, Losirian Isaaya, Dijalo
Kalalapapai, Paulo Tunyani, Mohamed Kinyonga na Daudi William.
Sajenti Munisi alidai kuwa watuhumiwa hao kwa
pamoja, waliwaua, Mussa Madola, Steven Kisichi, Masinga na Zungu Mgogo
katika kitongoji cha Mtanzania.
Alisema siku hiyo hiyo, , watuhumiwa pia waliwaua
Emmanuel Paul, Said Hamadi, Shukuru Paul, Mhaule Joseph, Zacharia Petro
na Rajabu Abdallah katika Kijiji cha Laitime.
Hata hivyo, washtakiwa hawakutakiwa kujibu lolote kwa sababu mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Februari 3 mwaka
Wakati huohuo, polisi wilayani humo, wamekamata
bunduki tatu aina ya Shortgun, Rifle mbili na bastola katika maeneo ya
mapigano kati ya wakulima na wafugaji wilayani humo.
Kamanda wa polisi mkoani Manyara, Akili Mpwapwa
alisema jana kuwa, katika operesheni yao, polisi pia wamefanikiwa
kukamata risasi 73.
Kamanda Mpwapwa alisema katika operesheni hiyo, watu 35 walikamatwa na 12 miongoni mwao wamefikishwa mahakamani.
Kwa mujibu wa kamanda huyo watu wengine 10 wapo chini ya uangalizi na saba wameachiwa huru
“Uchunguzi wa tukio hili, unaendelea na tuna imani wote waliohusika na mauaji watakamatwa,” alisema.
credit, mwananchi
0 comments:
Post a Comment