Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, Felchesmi Mramba
Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari juzi na Mkurugenzi
Mtendaji wa Tanesco, Felchesmi Mramba, ilisema wizi huo ulifanyika
Januari 10, mwaka huu katika kijiji cha Kakola B, Kata ya Kakola
wilayani Kahama na kusababisha usumbufu na hasara kubwa kwa wananchi,
mgodi wa dhahabu Bulyanhulu na shirika hilo.
Alisema mbali na hasara, hali hiyo imesababisha miji ya Shinyanga,
mgodi wa Bulyanhulu pamoja na mji wa Kahama kukosa huduma ya maji kwa
muda wa wiki mbili.
Kwa mujibu wa Mramba, nguzo zilizofanyiwa hujuma zimo katika njia kubwa ya umeme wa Kilowati 220.
Mramba ambaye alitembelea eneo la tukio ili kujionea shughuli
za ujenzi unaoendelea, alisema wizi huo utaisababishia shirika hasara
ya Sh. bilioni 3.5 ili kurejesha nguzo hizo.
Alisema nguzo iliyofanyiwa hujuma kubwa ni namba 266 na baada ya
kuanguka ilisababisha nguzo jirani, namba 277 pia kuanguka na
kusababisha kukosekana kwa umeme kwa wateja wanaotegemea laini hiyo.
0 comments:
Post a Comment