pagead2.googlesyndication.com pagead2.googlesyndication.com

Tanzania yaisambaratisha Kenya


Flag of Kenya.svg
Timu ya netiboli ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Queens imeibugiza Kenya magoli108-6 katika michuano ya Kombe la Mapinduzi inayoendelea kwenye uwanja wa Gymkhana, Zanzibar.
Katika mchezo huo, Kilimanjaro Queens inajivfunia kiwango kilichoonyeshwa na mchezaji Mwanaidi Hassan, aliyekuwa kinara wa kupachika mabao.
Katika mchezo mwingine, jahazi la Zanzibar lilizamishwa na Uganda baada ya kuwabugiza magoli 53-37.
Timu hiyo ya Tanzania Bbara ‘Kilimanjaro Queens’ itajitupa tena uwanjani leo jioni kucheza na Uganda, ukitanguliwa na ule wa asubuhi ambao utazikutanisha wenyeji Zanzibar atakabiliana na Kenya.
Mwenyekiti wa Chama cha Netiboli Tanzania (Chaneta) Anna Kibira alisema matokeo ya mchezo wa leo ndio yatakayoamua bingwa wa michuano hiyo.
“Baada ya mechi za leo tutahesabu pointi mbili mbili, atakayepata pointi nyingi ndio atakuwa bingwa michuana hii ya Mapinduzi,” alisema Kibira.
Kwa mujibu wa Sherry Khamis, Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Zanzibar (BMZ), michuano hiyo itafikia hatima yake leo.
“Michuano hiyo ni muhimu kwa nchi za kanda hii kwa vile zitasaidia katika maandalizi ya michuano mikubwa iliyo mbele yao baadaye mwaka huu.

0 comments:

Post a Comment